- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tarehe 11/8/2025, Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara alifanya Kikao kazi na watumishi wa Kabanga OSBP.
Lengo la Kikao kazi hicho ilikuwa ni kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja ya kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya forodha, utoaji bora wa huduma za hapo Mpakani na mapambano dhidi ya biashara haramu ya magendo toka nchi jirani.
Akiongea na watumishi hao Meneja TRA Mkoa wa Kagera ndg Castro John alisema TRA Mkoa wa Kagera imejipanga vema kuhakikisha inadhibiti biashara haramu ya magendo katika mipaka yetu ya Rusumo, Mugoma, Kabanga, Murusagamba na maeneo mengine ambayo hayana vituo vya forodha kama mpaka wa Tanzania na Burundi, mpaka wa Mugoma.
Aidha, ameagiza doria na operation mbalimbali ziendelee kufanywa na Kikosi maalum kitakachokuwa jukumu kubwa la kuhakikisha biashara na bidhaa zote toka nchi jirani zinapita katika mipaka rasmi na kwamba hakuna mfanyabiashara atakayeingiza bidhaa zake bila kulipa Kodi stahiki kwa mujibu wa sheria.
Mhe Col Mathias Kahabi DC Ngara amempongeza Meneja TRA Mkoa kwa elimu aliyoitoa katika mpaka wa Kabanga ambapo wakuu wa taasisi zote za Serikali waliopo mpakani hapo walihudhuria.
Ngara Kazi inaendelea.
www ngaradc go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa