- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
16/05/2025
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara alikutana na Brig Gen Gabriel E Kwiligwa - Kamanda Brigade ya Magharibi(202KV) kwa mazungumzo maalum ya Ulinzi wa mpaka wa Magharibi na nchi jirani tunazopakana nazo.
Mazungumzo hayo mafupi yalifanyika katika Mamlaka ya mji mdogo Rulenge.
Aidha, Brig Gen Gabriel E Kwiligwa ameridhishwa na shughuli za Ulinzi zinazofanywa na vikosi vyetu vya JWTZ vilivyoko mpakani kwa ajili ya Ulinzi na Usalama wa mpaka wetu wa Magharibi.
Pia Brig Gen GE Kwiligwa alimpongeza Kaimu Kamanda Kikosi 23KJ Maj Raphael L. Paschal kwa kazi nzuri ya kuhakikisha askari wa JWTZ walioko kwenye viteule sehemu mbalimbali wanatimiza wajibu wao kwa weledi, uhodari na nidhamu ya hali ya juu sana.
Afande Brig Gen Gabriel E Kwiligwa pamoja na shughuli ya Kutembelea mpaka pia alikuwa anatembelea viteule vya JWTZ kwa ajili ya kuwajulia hali maafisa na askari ili kuona hali ya utayari na pia kusikiliza na kutatua KERO zao.
Mwisho Mhe Col Mathias Kahabi DC Ngara, amemhakikishia Brig Gen GE Kwiligwa kuwa Wilaya ya Ngara ni salama na itaendelea kuwa salama kwa ushirikiano mkubwa uliopo kati ya vyomba vya usalama na wananchi wa Wilaya ya Ngara kwa ujumla.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa