- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 04/12/2025, Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara ametembelea Kiteule cha JWTZ kilichopo Kijiji cha Murusagamba, Kata ya Murusagamba Tarafa ya Murusagamba Wilayani Ngara.
Mhe Col Kahabi katika ziara hiyo alifuatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Kamati ya Usalama ya Kata/Tarafa ya Murusagamba pamoja na Mkuu wa Kiteule Maj Mzava.
Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kukagua shughuli za ulinzi na usalama zinazofanywa na maafisa na askari waliopo katika eneo la mpaka katika Kijiji na Kata ya Murusagamba.
Aidha, kwa niaba ya Kamati ya Usalama ya Wilaya Mhe Col Kahabi DC Ngara amewapongeza wananchi wa Kijiji na Kata hiyo kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa maafisa na askari wa JWTZ pamoja na vyombo Vingine vya ulinzi na usalama vilivyopo katika Kijiji na Kata hiyo inayopakana na nchi jirani ya Burundi.
Pia amewataka vyombo vyote vya usalama kushirikiana kuhakikisha hakuna wahamiaji haramu wanaoingia nchini mwetu kupitia njia ambazo sio rasmi(vipenyo) maarufu kama Panya road.
Amewakumbusha juu ya uwepo wa Task Force ambayo imeundwa tarehe 01/12/2025 na imeshaanza kazi ikiongozwa na OCD Ngara, DIO Ngara pamoja na maafisa na askari toka vyombo mbalimbali vya usalama Wilayani Ngara.

Ngara Kazi ya ulinzi na usalama inaendelea.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa