- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
15/01/2026
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara akifuatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Watalaam Mbalimbali toka H/W Ngara, Wakuu wa Taasisi za Serikali TARURA, RUWASA na TANESCO walifanya ziara ya Kutembelea Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kumpokea Mhe Hajjat Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa Kagera ambaye atafanya ziara Wilayani Ngara kuanzia tarehe 21-22/1/2026.
Miradi itakayotembelewa na Mhe RC ni pamoja na miradi ya elimu, afya pamoja na Kukagua ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa Mikutano uliopo Ngara mjini.
Aidha, Mhe Col Mathias Kahabi DC amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Mhe Dr Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuipatia H/W ya Ngara fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya Amali Kasharazi ambayo imeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza tarehe 13/1/2026.




Ngara Kazi inaendelea
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa