- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
28/03/2025
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara akifuatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Meneja ya TARURA Wilaya Eng Magori, Watalaam toka Ofisi ya TARURA pamoja na Viongozi wa Serikali wa Vijiji vya Muganza, Kibogora, Bukiriro na Rulenge tarehe 27/03/2025 walifanya ziara ya kukagua Barabara ya Kiusalama katika mpaka wa Tanzania na Burundi unaotenganishwa na mto Ruvuvu.
Mhe DC Kahabi kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Ngara anatoa pongezi nyingi kwa Mhe Dr Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuma pesa nyingi zinazoendelea kuboresha miundombinu ya barabara za vijijini zinazosimamiwa na TARURA.
Hali ya Barabara hizo ni nzuri na zinaendelea kutengenezwa ili kuungainisha wananchi vijijini waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi ikiwemo kusafirisha mazao yao kwenda kwenye masoko bila changamoto yoyote.
Aidha, DC Ngara Mhe Kahabi amemwagiza Eng Magori - Meneja TARURA Ngara kuweka kipaumbele katika matengezo ya barabara za kiusalama kurahisha shughuli za kiulinzi na Usalama wa mpaka wetu na jirani zetu.
Ngara Kazi inaendelea....
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa