- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 22/7/2025, Mhe Col Mathias Julius Kahabi na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya wamekutana na Viongozi wa Tembo Nickel na kumpa taarifa ya Maendeleo ya mradi huo.
Wakitoa maelezo ya mradi huo Dr Kudra Said - Kaimu Manager wa mradi wa Tembo Nickel na Ndg Ramson Msemakweli - Mkuu wa mpango wa Uhamishaji wa Makazi (Resettlement Action Plan Lead) kwa waguswa wa mradi huo wamesema mchakato wa kulipa fidia kwa vijiji vya Rwinyana, Bugara na Muganza uko hatua za mwisho za malipo hayo.
Aidha, baada ya kukamilika kwa mchakato huo viongozi na wananchi wa vijiji husika watataarifiwa rasmi na baadae kufanyika kwa mikutano ya kujenga uelewa wa pamoja kuhusu matumizi bora na sahihi ya fedha hizo.
Mhe Col Mathias Kahabi DC amewapongeza Viongozi hao kwa kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na mahusiano ya karibu na Serikali ya Wilaya.
Ngara kazi inaendelea.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa