• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

DKT. MWIGULU: KAZI ZINAZOWEZA KUFANYWA NA WAZAWA ZISIFANYWE NA WAGENI

Wakati ilipowekwa: January 14th, 2026

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amezitaka wizara zinazohusika na masuala ya ajira zisimamie kikamilifu utekelezaji wa sheria zinazotaka kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania zisifanywe na wageni isipokuwa zile zinazohitaji utaalamu ambao nchi inaupungufu.

Vilevile, Waziri Mkuu amekemea tabia ya baadhi ya wenye nyumba kumpangisha raia mmoja wa kigeni na kumruhusu mpangaji huyo apangishe watu wengine ndani ya nyumba hiyo jambo ambalo ni hatari kwa usalama na pia halina tija kibiashara. 

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Jumatano, Januari 14, 2026 alipofungua Kikao cha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara za Kisekta kujadili fursa za ajira ndani na nje ya nchi.

Agizo hilo linalenga kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la wageni kufanya kazi au biashara ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania na kuliwezesha Taifa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa ajira.

"Kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania ziachwe wafanye, si kuruhusu wageni wafanye. Tusioneane aibu kama tumefungua milango au kulegeza wataalamu wafuatilie. Wageni wafanye kazi za kitaalamu ambazo nchi ina uhaba wa wataalamu.”

Amesema kuwa ni lazima wataalamu wa ndani wasimamie sheria ipasavyo na kama kuna maeneo yanayokwamisha wayabainishe na yafanyiwe marekebisho. “Hatuwezi kuleta watu wanaokuja kufanya kazi ambazo Watazania wanaziweza.”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametoa wito kwa Watanzania kuwa na wivu na nchi yao kwa kutoruhusu baadhi ya vitu kufanyika, ambapo alitolea mfano suala la wenye nyumba kumpangisha raia moja wa kigeni ambaye naye analeta wenzake wengi katika nyumba hiyo hiyo.

“Watanzania tuwe na wivu na nchi yetu, mfano mtu anamkodishia nyumba mgeni kwa dola 5,000 kwa mwaka na kisha mgeni huyo anawaleta wenzake 60 na anawakodisha dola 500 hapo Mtanzania anapata hasara, hii si sawa hata kwa usalama.”

Waziri Mkuu amewaagiza wahusika wafuatilie suala hilo la makazi ili wakae katika utaratibu ulio rasmi. “Eneo hili liangaliwe wageni wanalundikana na kufanya kazi ambazo Watanzania wangeweza kufanya, hatuwezi kuruhusu hili tunataka wawekezaji.”

Hivyo, Waziri Mkuu ameziagiza wizara zinazohusika zifuatilie suala hilo, pamoja na kuwasisitiza wasimamie utekelezwaji wa sheria kwa sababu kila nchi ina sheria zake na Tanzania inatekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria.

Amesema sheria zimetungwa ili kusaidia kujenga kampuni za Watanzania na kuzikuza, hivyo wizara zinazohusika zihakikishe hazisajili kampuni za kigeni kabla ya kuzifanyia uchunguzi wa kina kwa sababu baadhi ya taarifa zinazowasilishwa si sahihi.

www.ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • DKT. MWIGULU: KAZI ZINAZOWEZA KUFANYWA NA WAZAWA ZISIFANYWE NA WAGENI

    January 14, 2026
  • RADIO KWIZERA YAZINDUA KAULI MBIU AMINIA 2026

    January 13, 2026
  • WAZIRI MKUU AONGOZA MKUTANO KAZI WA MAWAZIRI

    January 12, 2026
  • RAIS DKT. SAMIA: TUZO YA CAF INANIPA NGUVU YA KUANDAA AFCON 2027

    January 10, 2026
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa