- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) imeipatia shilingi 321,938,000.00, Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, kama fedha ya motisha kwa kujaza takwimu za mwaka 2018 na kukidhi vigezo, zitumike katika ujenzi wa miundombinu shule za msingi na sekondari.
Haya ameyasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara na Afisaelimu Ndugu Gideon Mwesiga, wakati wa kikoa cha wataalamu (CMT) Mei 15, 2019, wakati akiwakirisha mapokezi ya fedha hiyo katika kikao hicho.
“Idara ya Elimu Msingi na Sekondari tumepokea fedha hiyo, na katika barua ya katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), yenye Kumb. Na. DB, 291/298/3/47 ya Mei 10, 2019 imeelekeza matumizi ya fedha hiyo.” Alisema Ndugu Mwesiga.
Kadiri ya barua, asilimia 50 ambazo ni sawa na shilingi 160,969,000.00 zitatumika katika kukamilisha maboma na ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi, ambapo asilimia 50 ya fedha hiyo, imeingizwa moja kwa moja katika akaunti za shule zilizopata ufadhili huo.
Barua hiyo, imelekeza kuwa asilimia 20 sawa na shilingi 64,387,600.00, zitatumika kupanga ikama katika shule za msingi na za sekondari, ambapo asilimia 10 sawa na shilingi 32,198,800.00 zitatumika katika shule za msingi; huku asilimia 10 sawa na shilingi 32,198,800.00 itatumika kupanga ikama katika shule za sekondari.
Imeagizwa kwamba katika asilimia 10 ya fedha iliyotumwa ambayo ni sawa na shilingi 32,198,800.00; idara ya Elimu Msingi itatumia shilingi 16,096,900.00 katika ufuatiliaji na tathimini katika shule za sekondari na shilingi 16,096,900.00 kwa ajili ya shule za msingi,
Ndugu Mwesiga ameongeza kwamba barua hiyo imeagiza kwamba asilimia 10 sawa na shilingi 32,198,800.00; Idara ya Elimu Msingi itatumia kiasi cha shilingi 16,096,900.00, na idara ya Elimu sekondari shilingi 16,096,900.00 kwa ajili ya ukusanyaji wa takwimu.
“Tunaweza kusema kwamba Idara ya Elimu Msingi katika fedha ya motisha tumepata jumla ya shilingi 257,550,400.00 sawa na sasilimia 80, huku Idara ya Elimu Sekondari ikipata shilingi 64,387,000.00 sawa na asilimia 20 ya fedha iliyopokelewa kutoka program ya Lipa Kulinga na Matokeo (EP4R).” Alisema Ndugu Mwesiga.
Aidha, ameishukuru serikali kwa kuleta fedha hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, kwa kudai kwamba itapunguza changamoto za miundombinu katika shule hizo; huku akiishukuru kwa kuwapanga walimu 37 katika katika Halmashauri hiyo katika ajira mpya ya mwaka 2018/2019, ambapo kati yao walimu 06 pekee hawajalipoti katika vituo vyao.
Hata hivyo, Ndugu Mwesiga amefafanua kuwa kiasi cha fedha kilichopokelewa kimeshuka kutoka zaidi ya shilingi milioni 500 zilizopokelewa mwaka wa fedha wa 2017/2019 na kufikia zaidi ya shilingi milioni 300 katika mwaka wa fedha wa 2018/2019.
akifafanua sababu ya upungufu huo; amesema kwamba mwaka 2018 zaidi ya walimu 200, wamehama kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, na kusababisha ikama katika Idara za Elimu Sekondari na Msingi kupungua, kitendo kilichopelekea idara hizo kupata fedha pungufu, ikilinganishwa na fedha iliyotolewa mwaka 2017/2018 wa fedha.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa