- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
17/03/2025
Imefanyika Jogging na Mazoezo ya pamoja kwa watumishi na Wananchi Ngara mjini.
Jogging ambayo huanzia uwanja wa Mpira wa kikapu Ngara mjini kuanzia saa 12 affajri Watumishi na Wananchi walijitokeza kwa ajili ya kujenga afya ya mwili , ambapo Mazoezi huleta umoja ,ushirikiano na mshikamano .
Kauli mbiu ikiwa "kuzeheka ni lazima lakini kuchakaa ni hiari yako fanya fanya Mazoezi "
Akiongea baada ya Jogging na mazoezi ya pamoja kamanda Kisaka ambaye alimwakilisha ocd alisema Mazoezi ni Muhimu kwa mwili wa Mwanadamu hivyo alisisitiza kuendelea bila kuacha pia amewataka wanamazoezi kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi inatokea tatizo mfano uhalifu.
Naye Ndg Said Salum kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya alisisitiza kufanya mazoezi angalau kila siku dk 30 na kuendelea aidha alitaja faida mbalimbali za kufanya mazoezi na hasara za kutokufanya mazoezi ikiwa na magonjwa nyemelezi BP, Sukari .
Aliendelea kwa kusema tuna Ngara fitness ambao hufanya mazoezi siku za Jumatatu ,Jumatano Alhamis na ijumaa Ngara mjini. Lakini pia kuna Ngara Jogging Club kila Jumamosi .
Ngara kazi inaendelea
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa