- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
19/07/2025
Imefanyika Jogging ,Mazoezi ya pamoja( Aerobic) na Bonanza la michezo ya kuvuta kamba na Soka Mbuzi wa Bahati ambaye ni Afisa Utumishi katika Halmashauri ya wilaya.
Katika mchezo wa kuvuta kamba wanaume kati ya Watumishi Vs Wananchi na matokeo watumishi waliweza kushinda na kupata kuku Jogoo pia kamba wanawake watumishi waliweza kuwashinda Wananchi .
Mgeni rasmi katika Jogging na Bonanza alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Bi Jenifer Mapembe ambaye ni Mkuu wa idara ya utawala na usimamizi wa Rasilimali watu.
Jogging ilishirikisha watumishi wa Serikali taasisi na Mashirika,wafanyabiashara ,wanachuo cha Nersing Murgwanza ,wakulima ,wafufugaji na wajasiliamali wadogowadogo (Wananchi)
Katika Bonanza la Soka (Mbuzi wa Bahati ) lililoshirikisha jumla ya timu sita 6 ambapo
Timu ya Ngara Boys imeibuka Bingwa na kujinyakulia zawadi ya Mbuzi wa Bahati katika Bonanza lilofanyika uwanja wa Posta Ngara Mjini baada ya kuifunga timu ya Nursing FC ya Murgwanza kwa Mikwaju ya Penalty 7-6 baada ya kumalizika 0:0 kwa dakika 90 za Mchezo.
Jogging ya pamoja
Jogging ikiongozwa na Mkiti Dr Mapunda
Jogging Club Ngara Mjini ambayo hufanyika kila Jumamosi kwa ajili ya kujenga afya ,mshikamano ,urafiki ,umoja ,mahusiano ,amani na upendo
Baada ya kumaliza Jogging
Mazoezi ya pamoja katika uwanja wa mpira wa kikapu Ngara mjini
Kaimu Ded Bi Jenifer Mapembe baada ya kutoa zawadi ya kuku kwa mshindi wa kamba katika uwanja wa mpira wa kikapu Ngara mjini
Waamuzi waliochezesha Bonanza soka ( mbuzi wa Bahati Afisa utumishi)
Wanamichezo wa Bonanza la soka katika uwanja wa posta ya zamani wakimsikiliza Mgeni Rasmi Kaimu Ded Bi Jenifer Mapembe akitoa neno kabla ya kuanza Bonanza hilo.
Mchezo wa kuvuta kamba kati ya watumishi na Wananchi
Mbuzi akikabidhiwa kwa captain wa timu ya Ngara Boys na Muandaaji soka Bonanza Bw Bahati Marco ambaye ni Afisa utumishi Katika Halmashauri ya wilaya akiwa na Afisa Utamaduni sanaa na Michezo Ndg Said.H.S
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa