• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

KAGERA INA KILA SABABU YA KUKUA KIUCHUMI

Wakati ilipowekwa: August 12th, 2019

Wiki ya uwekezaji Kagera imefunguliwa leo tarehe 12 Agosti 2019 katika Ukumbi wa ELCT ulioko Manispaa ya Bukoba . Mwenyekiti alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali  Marco E. Gaguta. Kongamano hili lilihudhuriwa pia na Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Congo, Rwanda,Uganda,Burundi na Kenya. Wakuu wa Wilaya zote za Kagera,Makatibu Tawala ,Wakurugenzi, Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali walihudhuria  pia.

Mkuu wa Mkoa alisema,"Mkoa wa Kagera umebahatika kuwa na fursa nyingi za kiuchumi. Nchi ya Tanzania imepakana na nchi sita ambazo inaweza kufanya nazo biashara moja kwa moja ambapo Kagera peke yake inapakana na nchi nne yaani Congo, Rwanda, Burundi na Uganda. Hivyo Kagera inatakiwa kuwa  jukwaa la kufungua milango ya kuelekea kufikia soko la ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania".

Baada ya kufungua kongamano hilo,Mkuu wa Mkoa alitoa rai kwa wafanyabiashara kuitumia vyema fursa ya kupakana na nchi hizo nne kukuza uchumi wa kagera na Taifa kwa ujumla.

Katika uwasilisho wa taarifa za fursa zinazopatikana nchini Burundi,Balozi wa Tanzania nchini Burundi  Dr. Edmund  aliwataka wafanyabiashara kujenga,kudumisha na kutumia mahusiano vizuri na wafanyabiashara wa Burundi maana Burundi inategemea sana bidhaa kutoka Tanzania. Hivyo Burundi itakuwa soko la Tanzania.

Balozi wa Tanzania nchini Congo  Lt. Jen. (Mstaafu) Paul I. Mella wakati wa taarifa yake alieleza kuwa Tanzania tuna fursa kubwa ya soko la mazo na bidhaa nyingi za viwandani. Pia aliwatoa hofu wafanyabiashara juu ya hali ya usalama na amani nchini Congo na kudai kuwa hali ni shari na salama hivyo wafanyabiashara wasipate hofu.

Balozi wa Tazania nchini Uganda Mh, Dk. Aziz P. Mlima alizungumzia fursa ambazo tunaweza kuzitumia nchini humo ikiwemo zao la parachichi ambalo Kagera tuna ardhi nzuri ya kustawi zao hilo. Pia alialika wawekezaji kuja kuwekeza katika sekta ya utalii mkoani Kagera maana ina vivutio vya muhimu na vya kuvutia.

Balozi wa Tanzania nchini Kenya aliwaomba vyama vya biashara ikiwemo TCCIA na taasisi zingine za kibiashara ziwe msaada mkubwa kwa kutoa elimu juu ya ufanyaji wa biashara za kimataifa ikiwemo kufuata taratibu za nchi hizo.Balozi huyo alisema,"Kabla ya kuchukua fursa nchi za jirani au za nje ,wafanyabiashara mfanye takwimu,utafiti na kufuata taratibu za kibiashara katika nchi hizo ili kukwepa usumbufu".

Balozi wa Tanzania nchini Rwanda naye aliomba kujengwa kwa masoko ya mpakani ili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za wenda nchi jirani kwa ukaribu.

Mwisho Mwenyekiti wakati akihitimisha,aliwashukuru Mabalozi kwa kuitikia mwaliko huo wa kuja kuelezea wafanyabiashara juu ya fursa zilizopo nchi hizo.Pia aliwaomba kuyafanyia kazi maneno yaliyoletwa na mabalozi pamoja na kujipanga kwa ajili ya kufanya ziara ya kwenda kutembelea nchi jirani kwa dhumuni la kujionea fursa hizo.Alimaliza kwa kusema,"Maneno pekee bila matendo hatuwezi kufika popote'.

KAGERA:Eneo La Kimkakati Kwa Uchumi Wetu Na Afrika Mashariki

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • DC NGARA MHE COL MATHIAS KAHABI AKUTANA NA BRIG GEN GABRIEL E. KWILIGWA - KAMANDA BRIGDE YA MAGHARIBI.

    May 16, 2025
  • MHE COL MATHIAS JULIUS KAHABI DC NGARA ASHIRIKI USAFI NA WANANCHI WA NAKATUNGA

    May 15, 2025
  • MWENYEKITI WA CCM AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO - NGARA

    May 16, 2025
  • KIKAO KAZI CHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AFUA ZA LISHE WA KILIMO CHA MAHINDI CHAFANYIKA - NGARA

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa