- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamati za Ukimwi Mkoani Kagera zimetakiwa kuwahamasisha na kuwahimiza wananchi waendelee kupima Virus vya Ukimwi, kwa lengo la kujua afya zao. ili wajiepushe na maabukizi ya ugonjwa huo.
Haya ni kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen. Marco Elisha Gaguti katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, iliyosherehekewa Kimkoa Wilayani Ngara Desemba 01, 2018.
“Wananchi tujitokeze kupima afya zetu, tukilenga kufikia lengo la Dunia la90% ya watu wote wawe wamepime virus vya ukimwi, 90% ya watu wawe wanatumia ARV, na 90% watu wawe wamefubaza virus vya ukimwi ili wawsiwe na uwezo wa kuambukiza.” Alisema Lt. Col. Mntenjele.
Lt. Col. Mntenjele amesema kwamba kamati zinawajibika kutoa elimu na hamasa kwa wananchi, ili kwa hiari yao wakapime virus vya ukimwi, kwa madai kwamba wakishajua afya zao, watajilinda kwa kufuata maelekezo ya wataalamu.
Amezitaka kamati za ukimwi kushirikiana na mashirika yanasaidiana na serikali kuthibiti kuenea kwa virus vya ukimwi, kuwaelimisha wananchi wajitokeze kwa hiari kupima virus vya kwa lengo la kudhibiti gonjwa hili hatari.
Aidha, amesema kitaifa takwimu zinaonyesha kwamba Januari – Oktoba 2018; watu 1,291,735 walipima virus vya ukimwi, kati yao 16,048 sawa na 1.2% walikuwa wameambukizwa virusi vya ukimwi, ikilinganishwa na Januari – Desemba 2017 ambapo maambukizi yalikuwa 1.6%.
Katika Mkoa wa Kagera takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi tangu Januari hadi Oktoba 2018; Wilaya ya Missenyi ilikuwa na 1.8%, Ngara 0.5%, Muleba 1.7%, Bukoba Manispaa 1.7%, Bukoba Vijijini 1.7%, Kyerwa 1.2%, Biharamulo 1.0 ambapo Karagwe maambukizi yalikuwa 1.0%.
Amewakumbusha wananchi wa Wilaya ya Ngara wasijivune kwa takwimu hizo, kwani wanopima afya zao ni wale wanaojiamini, huku akisdai kwamba wasiopima ni wale wenye mashaka na afya zao; kwa hiyo, mtu atajua yuko salama au la kwa kupima na si vinginevyo.
Wakti huo huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amani Anasitazi Mpanju, amesema maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, yanaagukia katika siku 16 zinazolenga kupinga ukatili dhidi ya wanawake, watoto na makundi mengine katika jamii.
“Nimejumuika katika maadhimisho haya, kwa sababu tunapoongelea kupinga ukatili dhidi ya ya makundi ya wanawake, watoto na wengine katika jamii yetu, hatuwezi kukwepa sekta ya sheria, ambayo wizara yangu ndiyo yenye dhamana.” Alisema Ndugu Mpanju.
Wizara ya Katiba na Sheria inaelekezwa kuhakikisha makundi ya pembezoni, ikiwemo watu wanaoishi na virus vya ukimwi, wanapata huduma ya msaada wa kisheria, ili waweze kupata haki zao pasipokuwa na vikwazo vyovyote.
Amesema yapo makundi kwa muda mrefu wamekuwa hawapati haki zao, kwa sababu ya gharama za kuwalipa mawakili waweze kupata haki, na moja ya makundi hayo ni watanzania wanaoishi na virus vya ukimwi.
Kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yamefanyika kimkoa Wilayani Ngara na kuhudhuliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndugu Amani Anastazi Mpanju, Mganga mkuu wa Mkoa wa Kagera Dr. Marco Mbata, Mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na viongozi wa wilaya ya Ngara.
Pia Maadhimisho hayo yamefutia wananchi kwa hiari kupima afya zao, kupata ushauri nasaha, wa kisheria na hata kufanya tohara kwa vijana na wanaume wenye umri wa miaka 18 na kunedelea; ambapo Kauli mbiu ya katika maadhimisho hayo inasema; “Pima, Jitambue, Ishi.”
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa