- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo Septemba 07, 2025
Mwenge wa Uhuru umepokelewa katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Nyakabango Wilayani Muleba ili kuanza mbio zake katika Mkoa wa Kagera ukitokea Mkoa wa Geita.
Akiongoza mapokezi hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoa wa Kagera Utakimbizwa umbali wa Kilomita 1,040 na utatembelea, utazindua, utafungua na kuweka mawe ya Msingi katika Miradi 58 yenye thamani ya shilingi bilioni 23.8.
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri zote nane ambazo ni Muleba, Bukoba Vijijini, Bukoba Manispaa, Missenyi, Kyerwa, Karagwe, Ngara na Biharamulo.
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuhitimisha mbio zake tarehe 15 Septemba 2025 na kukabidhiwa katika Mkoa wa Kigoma.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2025 ni "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu".
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa