- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATE
15/03/2025
Mkiti wa umoja wa Wafanyabiara Ngara Ndg Chrispine Kamugisha na ameongoza msafara wa kuelekea Wilaya ya Kirehe Mkoa wa Kibungo nchini Rwanda .
Mkiti huyo ameongozana na kaimu Afisa Biashara Viwanda na uwekezaji Ndg Privanus Katinhila Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya, na wafanyabiashara zaidi ya 80, kutoka Ngara.
Lengo la kikao hicho ni kubadilishana Mawazo kibiashara , ambapo kiongozi wa kirehe aliwaomba kushirikiana na tayari wamejenga soko kubwa wanawakaribisha wafanyabiashara toka Ngara Tanzania.
Nae Ndg *Chrispine kamugisha Mkiti wa wafanyabiashara Ngara* aliwaambia kuwa wafanyabiashara Ngara wamefika na bidhaa za maonesho zilizoletwa na wafanyabiashara kutoka Ngara Tanzania waone ambapo walivutiwa sana na vitu hivyo pia aliwajulisha lipo soko la kimkakati kahaza Rusumo lipo hatua ya mwisho kukamilika aliwakaribisha wafanyabiashara wa Rwanda kuja kuwekeza katika soko hilo jipya.
Aidha Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Privanus katinhila Amesisitiza umuhimu wa falsafa ya 4R ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasani na kupongeza mashirikiano yaliyoasisiwa na Mhe. Rais Paulo Kagame na Mama Samia S.H amemalizia kwa kusisitiza ushiriki wa Wafanyabiashara wanawake katika biashara za mipakani
Aidha Naye Mkuu wa Wilaya ya kirehe amewapongeza Waheshimiwa Maraisi wa Rwanda Paul Kagame na Tanzania Dkt Samia Suruhu Hassani kwa ushirikiano wao mkubwa katika nchi hizi Mbili.
Baada ya kikao ulifanyika Mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya timu ya Rusumo F.C Ngara Tanzania na Imena FC kirehe Rwanda huku timu ya Imena FC ikiibuka na
Mshindi kwa magoli 2 kwa 1 dhidi ya Rusumo FC ambapo ilinyesha mvua kubwa na kusababisha uwanja kuwa na tope, utelezi.
Picha ya pamoja viongozi wa Kirehe na Ngara katika kikao hicho kilichofamyika ukumbi wa wilaya Kirehe mkoani kibungo Rwanda
Wafanyabiashara wa Ngara na kirehe katika kikao
Bidhaa za maonesho kutoka Ngara
Timu ya Rusumo Fc toka Ngara
Timu ya imena Fc ya Kirehe
Ngara kazi inaendelea
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa