- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
1/12/2025
Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kwa mwaka 2025 wilayani Ngara yalifanyika katika kata ya Kasulo, kijiji cha Rwakaremela kwa kuanza kutoa elimu ya VVU na UKIMWI, Athari za Mimba katika umri mdogo, Uundaji wa Klabu za kupinga UKIMWI na Mimba za utotoni kwa Shule ya Sekondari Rusumo na shule ya Msingi Njia panda tarehe 28 hadi 30/11/2025, na tarehe 1.12.2025 siku ya kilele huduma zilizotolewa ni:-
1. Kutoa elimu ya VVU na UKIMWI katika Jamii hasa kwa makundi ya vijana na wanandoa.
2. Athari za ugonjwa wa UKIMWI na unyanyapa katika familia, Jamii na taifa kwa ujumla.
3. Huduma za ushauri nasaha na upimaji VVU kwa hiari.
4. Uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana na wanawake ambayo ilikuwa ikitolewa katika zahanati ya Lourdes.


Kauli Mbiu Katika Maadhimisho hayo ilikuwa ni SHINDA VIKWAZO , IMARISHA MWITIKIO TOKOMEZA UKIMWI.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa