- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
Mtoto wa miaka 10 aliyeteseka na uvimbe kinywani kwa zaidi ya miaka sita (6) kwa kukosa fedha za kufanyiwa upasuaji, leo Novemba 6, 2024 amefanyiwa upasuaji na Madaktari Bingwa wa Rais Samia, kuuondoa uvimbe huo katika Hospitali ya Nyamiaga, wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Akizungumzia upasuaji huo Daktari Bingwa wa kinywa, meno, taya na sura kutoka Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo Dar es Saalam, Dkt. Beatus Msemakweli baada ya kufanikisha upasuaji huo amesema wazazi wa mtoto huyo wamesumbuka kwenda katika hospitali mbalimbali kutafuta matibabu hadi nchi jirani ya Burundi lakini bila mafanikio.
"Sasa baada ya kusikia kuwa Madaktari wa Samia tupo hapa na yeye akajitokeza kuja kupata matibabu na tumemfanyia upasuaji tayari yupo wodini anaendelea vizuri chini ya uaangalizi," ameeeleza Dkt. Msemakweli.
Aidha, Dkt. Msemakweli amesema pamoja na matibabu hayo wanayotoa kwa wananchi, pia wanatoa ujuzi kwa wataalamu walipo katika hospitali za wilaya ili hata watakapoondoka huduma hizo ziendelee na kupunguza rufaa.
Madaktari hao wameweka kambi katika hospitali nane (8) za wilaya za mkoa Kagera kwa lengo la kuboresha huduma za kibingwa na bingwa bobezi pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wa afya katika ngazi ya Msingi.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa