- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mafunzo yameendelea Kwa watendaji wakata, vijiji , maafisa elimu kata , Wakuu wa shule, walimu wakuu, Wakuu wa vituo vya afya , maafisa Kilimo kata na maafisa Maendeleo ya jamii kata.
Mafunzo hayo yanayotolewa na viongozi kutoka ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma yaliyoanza tarehe 10/12/2023 na Kutolewa Kwa wakuu wa idara, Vitengo na Wasaidizi wao.
Akiongea Mkurugenzi Msaidizi ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma Bi Jeanfrida B. Mushumbuzi. Alisema mfumo wa Usimamizi wa utendaji kazi katika utumishi wa Umma PEPMIS/ PIPMIS Ndani na nje utawezesha.
Kuchochea na kuleta mageuzi Makubwa katika usimamizi na upimaji wa watendaji katika utumishi wa Umma.
Kuchochea utumishi wa Umma unaofanywa kazi Kwa Weledi,bidii na uadilifu.
Ambapo alisema utumishi wa Umma unawajibika Kwa Umma wa Watanzania unaojali utendaji kazi wenye matokeo Kwa wakati, unatenda haki na unazongatia na uzalendo wa kitaifa ili kuimarisha utoaji Huduma Bora Kwa wananchi.
Nae kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg.Constantine Msemwa aliwaka wanamafunzo wote kuwa wasikivu Kwa mada Mbalimbali zitakazofundishwa ikiwa na kufanya Kwa usahihi zoezi la kuingia kwenye mfumo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Constantine Msemwa akiwa na Afisa utumishi Ndg Bahati Marco ,pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma Bi Jeanfrida B. Mushumbuzi na viongozi wengine Toka Ofisi hiyo.
Wanamafunzo kutoka kata 22 za wilaya ya Ngara wakiwa kwenye ukumbi wa St Francis.
Wanamafunzo maafisa elimu wakiwa na Afisa elimu Msingi Bi Josline Bandiko.
Wanamafunzo wakiwa na Afisa elimu Sekondari Mwl Enock Ntakisigaye.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa