- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
05/08/2025
Mafunzo hayo yameendelea kufanyika ikiwa ni siku ya pili katika ukumbi Wa Community Centre Ngara Mjini .Ambapo walianza na Marejeo ya mada zilizofundishwa siku ya kwanza.
Mada zilizofundishwa ni
1.Taratibu za Upigaji kura ambapo mada iliwezeshwa na Ndg Telespord Ngerangera.
2. Mazoezi ya ufungaji Vituturi na masanduku ya kura, matumizi ya Majalada ya Nukta Nundu na kutazama picha za video (video clips) kuhusu Upangaji sahihi wa kituo, Ufungaji wa kituturi,kufunga masanduku ya kura na Namna ya kufunga karatasi ya kura.Mada iliyowezeshwa na Ndg Jacob Sona
3. Taratibu za kuhesabu kura kituoni na kutazama picha za video kuhusu kuruhusiwa kuwepo katika chumba cha kuhesabia kura, Utaratibu wa kufungua masanduku na aina za kura ambapo mada iliwezeshwa na Ndg Josephat Sangatati
4.Kujumlisha kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani pia kutazama picha za video kuhusu Maandalizi katika Sehemu ya kujumlisha kura,Utaratibu wa kufuatwa kabla ya kujumlisha kura ambapo mada hiyo iliwezeshwa na Bi Sakina Chamiti.
5. Fomu zinazotumika wakati wa kupiga kura ,kuhesabu kura, na kujumlisha Matokeo na Mazoezi ya kujaza fomu kwa vitendo mada hii iliwezeshwa na Bi Josephina Lusatira
Aidha yalifanyika Majadiliano kulingana na Mada iliyofundishwa.
www ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa