- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
Leo tarehe 11/11/2024, Meneja RUWASA Wilaya ya Ngara Eng.Simon Ndyamukama amemtambulisha Mkandarasi wa Miradi ya Maji Ofisini kwa DC Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi.
Miradi hiyo itaanza kutekelezwa hivi karibuni na Mkandarasi Audacia Investment Ltd katika Vijiji vya Kumubuga na Ntanga kwa gharama ya Tsh. 1,347,213,894.20. Mradi huu unatekelezwa kwa miezi 8 na unatakiwa kukamilika tarehe 12/06/2025. Shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi wa tenki la Lita 120,000, matenki mawili kila moja Lita 75,000, Nyumba ya mitambo na ufungaji pampu ya sola, vituo vya kuchotea maji (DP) 6, Ofisi ya CBWSO na mtandao wa Bomba 24.2km.
Aidha, Mkandarasi Audacia Investment Ltd atatekeleza Mradi mwingine katika Kijiji cha Katerere kwa gharama ya Tsh. 1,166,537,161.70. Mradi huu unatekelezwa kwa miezi 8 na unatakiwa kukamilika tarehe 12/06/2025. Shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi wa chanzo, ujenzi wa tenki la Lita 150,000 juu ya mnara wa 6m, tenki la kupokea maji (sump tank) la Lita 120,000, ukarabati wa Nyumba ya mitambo na ufungaji pampu ya umeme, ukarabati wa vyanzo viwili, vituo vya kuchotea maji (DP) 8, Ofisi ya CBWSO na mtandao wa Bomba 20.7km.
Mhe Dc Col Mathias Kahabi kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Ngara, Ametoa pongezi na shukrani nyingi kwa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha nyingi ya kutekeleza miradi ya maji na Miradi mingine mingi katika Sekta mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Ngara Kazi inaendelea...
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa