- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe Col. Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara leo tar 03 Disemba, 2025 amefanya kikao kazi na viongozi Dini.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya kikijumuisha viongozi kutoka Madhehebu mbalimbali ya kidini ambao wamekutana na kubadilishana mawazo juu ya namna bora ya kudumisha maelewano, mshikamano na utulivu wa Jamii.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Col. Kahabi amesisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa ustawi wa wananchi na maendeleo ya wilaya,
"Ngara imekuwa mfano wa maeneo yenye utulivu na mshikamano. Ili tufike mbali zaidi, tunahitaji ushirikiano wa dhati kati ya Serikali na taasisi za dini" amesisitiza Col. Kahabi
Kwa upande wao, viongozi wa dini wameipongeza Serikali inayoongozwa na Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasaidizi wake kwa utaratibu wa kuwaleta pamoja na kuwashirikisha katika masuala muhimu yanayoigusa jamii, huku wakiahidi kuendelea kuwa mstari wa mbele kuhimiza amani, upendo na uvumilivu miongoni mwa waumini na wananchi kwa ujumla.



Ngara, Amani ndiyo Msingi wetu
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa