- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 02/10/2025,
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara ametembelea ujenzi wa barabara ya Kivukoni Rusumo katika mto Ruvuvu ambayo inaendelea kujengwa na Mkandarasi Kika Construction company Ltd.
Ujenzi wa barabara hiyo ulianza mwezi June 2025 na unatarajiwa kukamilika mapema mwezi October 2025 kulingana na Mkataba.
Barabara hiyo inayounganisha mji wa Ngara na Kata za Ngara Mjini, Murukulazo, Rusumo na Kata zingine jirani kukamilika kwake itaondoa Kero kubwa ya kutopitika iliyokuwepo hususan wakati wa msimu wa mvua.
Aidha, barabara hiyo itakuwa kichocheo kikubwa cha uchumi wa wananchi wa Kata hizo ambao muda mwingi hutumia katika usafirishaji wa mazao yao toka sehemu moja kwenda nyingine.
Mhe Col Mathias Kahabi kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Ngara anapenda kutoa shukrani nyingi kwa Mhe Dr Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusikiliza na kuondoa KERO hiyo ya muda mrefu.
Pia Mhe Col Kahabi amepongeza kazi kubwa anayoifanya Mkandarasi Kika Construction company Ltd na kumtaka amalize ndani ya muda uliopo kwenye Mkataba.
Ngara kazi inaendelea.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa