- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
Tarehe 09/2/2025
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara akifuatana na Mbunge Jimbo la Ngara Ngara Mhe Ndaisaba George Ruhoro, Mhe Annna Amas - Katibu wa CCM(W) Mhe Yusuph Katura - Diwani Kata ya Kasulo pamoja na Viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wa Kijiji/Kata na Wilaya walifika katika Kitongoji cha Kamuli, Kijiji cha Rwakaremela, Kata ya Kasulo kwa ajili ya kuwafariji na kuwapa pole familia ya Mgane Emily Abel ambaye mke wake Bi. Emeriana Yona aliuawa na Tembo usiku wa kuamkia tarehe 09/2/2025.
Marehemu bi. Emeriana Yona aliuawa na Tembo wakati akijaribu kuwafukuza kundi la Tembo waliokuwa wamevamia shamba lao la mahindi. Katika jitihada hizo marehemu Emeriana alishambuliwa na Tembo hao hadi umauti ulipomkuta.
Pamoja na maelezo ya Viongozi mbalimbali akiwemo Mhe Mbunge Ndaisaba George Ruhoro, Mhe DC Col Mathias Kahabi anawapongeza sana Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na wananchi kwa kuungana pamoja kutoa salamu za rambirambi kufuatia msiba huo. Pia amemuagiza Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Burigi - Chato kuzifanyia kazi changamoto nyingi zinazowagusa wananchi wa Kata ya Kasulo wanaoishi karibu na Hifadhi ya Burigi - Chato.
Kwa muda mrefu sasa Tembo wamekuwa wakivamia mashamba ya wananchi wa Kata ya Kasulo na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazao ya wananchi na hata kusababisha vifo kwa wananchi wanaojitoa kulinda mazao yao bila kufuata tahadhali rafiki za kiusalama.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa