- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
05/12/2025
Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Dotto Jasson Bahemu, amefanya ziara katika Hospitali ya wilaya ya Ngara, Mbuba, ili kuona maendeleo ya ujenzi wake.
Akiwa Hospitalini hapo, Mhe. Dotto amesema amefika Hospitalini hapo, kuona maendeleo ya ujenzi wake, ili aweze kuongea na Wizara husika kuomba fedha za umaliziaji wa baadhi ya miundombinu ili kuwezesha upatikanaji wa huduma zote muhimu.
Akiwa Hospitalini hapo, Mhe. Dotto amewasihi Watumishi kutoa huduma nzuri na kuwajali Wananchi, ili kutafsiri vyema maono ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa Wananchi.
Katika ziara hiyo, Mhe. Mbunge aliongozana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ngara Ndg. Vitalis Ndairagije, DR Degrathias Mlandali Mganga Mkuu kny Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ,Diwani wa Kata ya Mbuba Mhe. Michael Bundora, Diwani wa Kata ya Rulenge Mhe. John Fabian Banigwa, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Ngara ambayo inasimamia Elimu na Afya Ndg. Abdallah Kirobi, pamoja na baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Kata ya Mbuba.




www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa