- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
12/01/2026
Uongozi wa Radio kwizera umefanya maombi na uzinduzi wa kauli mbiu 2026 ambayo ni AMINIA.
Maombi yaliongozwa na Baba Askofu Severine Niyomugizi (RC) Aidha katika uzinduzi huo alishiriki Ndg.Said Salum K/Mkuu kitengo cha utamaduni sanaa na michezo pia (Mawasiliano Serikalini) aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Solomon O.Kimilike Mgeni rasmi.
Katika tukio hilo uongozi wa Rk pamoja na watangazaji wote walishiriki kikamilifu tukio hilo.taarifa ya uzinduzi ilitolewa na Bi Zawadi Bashemela ambapo kipindi cha asubuhi njema uzinduzi wa kauli mbiu kiliongozwa na Bi Joyce Avile.
Pia Bi Flora Nyambi afisa utamaduni na michezo alishiriki katika uzinduzi.
Adha uongozi wa RK upo tayari kwa ushirikiano na Halmashauri kuwa na vipindi kwa Idara na vitengo kupitia Asubuhi njema pia kutangaza habari za uhakika yanahofanywa na serikali kupitia Halmashauri.
Naye mwakilishi wa Mkurugenzi Ndg said amewaeleza menejiment ya RK kuwa Halmashauri itatoa ushirikiano mkubwa kupitia Idara zake ili kuwaabarisha wananchi habari mbalimbali hasa za maendeleo zinafofanywa na Serikali kupitia Radio Kwizera ambayo husikika zaidi ya Mikoa Mitano 5.




www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa