- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo Tarehe 10/12/2024, Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara amekutana na Waislam wa Kijiji cha Kumubuga Kata ya Nyarmagoma na kumaliza mgogoro wa kiwanja kati ya Taasisi ya JASUTA na BAKWATA uliodumu kwa muda mrefu.
Viongozi wa Taasisi zote hizo mbili ngazi ya Wilaya wakiongozwa na Shehe wa Wilaya - (BAKWATA) - Alhaj Rajab Msabaha kwa pamoja wameridhia kumaliza mgogoro huo na kuahidi kutotokea tena kwa maslahi mapana ya waumini wao na jamii kwa ujumla inayowazunguka.
DC Ngara Mhe Col Mathias Kahabi, amepongeza hatua hiyo na kuwashukuru sana Viongozi hao ngazi ya Kijiji, Kata na Wilaya kwa utayari na uamuzi wa kumaliza mgogoro ambao ulikuwa changamoto kubwa kwa wananchi na waumini wa eneo hilo.
Ngara Kazi inaendelea....
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa