- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
27/12/2024
Mhe. Col Mathias J Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara amefanya ziara kukagua barabara ya Kumuyange – Mugasha – Murunyinya yenye urefu wa KM. 13.3 pamoja na Mradi wa maji wa Kumuyange Kata ya Nyamiaga na Kigina Kata ya Ntobeye.
Katika Ziara hiyo ameambatana na Afisa Tarafa Nyamiaga Bw. Jawadu Yusuph, Kaimu Meneja wa TARURA Bw. Emmanuel ndalihaze, na Afisa Mtendaji wa Kata ya Murukulazo Bw. Julian mwesiga. Kutoka Ofisi ya Meneja wa RUWASA Wilaya ya Ngara aliambatana na Bw. Rashid Omar Mwalimu na Bw. Innocent Medard Kahaya.
kwa upande wa Barabara ya Murunyinya hadi Kumuyange yapo maeneo ambayo yameharibika na yanahitaji matengenezo hususani kipande cha Barabara kuanzia Murunyinya hadi shule ya msingi Bulengo.
Kaimu Meneja wa TARURA amemueleza Mhe. Col Kahabi Mkuu wa Wilaya kuwa katika mwaka wa fedha 20224/2025 TARURA Wilaya ya Ngara kupitia fedha ya Mfuko wa Jimbo iliingia Mkataba na Mkandarasi Chomola Technical (T) Ltd Mkataba na. 510/006/2024/2025/W/22 kutengeneza matengenezo ya kiwango cha changarawe urefu wa KM. 2 kwa gharama ya Tshs. 42,715,500.00 katika matengenezo haya eneo litakalotengenezwa ni kuanzia Shule ya Msingi Mugasha hadi kwenye senta ya Chamukube.
Ameeleza pia Katika mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 TARURA Wilaya ya Ngara imetenga pia kiasi cha Tshs. 25,000,000.00 kupitia bajeti za fedha za Mfuko wa Jimbo itatengeneza kipande cha urefu wa KM. 1 kwa kiwango cha changarawe na kujenga Calvati moja eneo ambalo Barabara imekatika.
Baada ya bajeti kupitishwa Ofisi ya TARURA itapita tena kwenye Barabara hiyo ili kubaini maeneo ambayo yameharibika kwa ajili ya kufanya makisio ili yaweze kutengenezwa.
Kwa upande wa Mradi wa maji Kumuyange/ Kigina amekagua utekelezaji wa Mradi huo unaotekelezwa na Mkandarasi Buzubona & Sons Co. Ltd kwa thamani ya Tshs. 1,669,188,309.52. Utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 20 na unatarajiwa kukamilkika ifikapo tarehe 10/03/2025. Aidha kukamilika kwa Mradi huu utawanufaisha Wananchi wapatao 2000 wa Kitongoji cha Kumuyange.
Shughuli zilizotekelezwa mpaka sasa ni ujenzi wa chanzo, Ujenzi wa tenki lita. 25,000 na ujenzi wa tenki lita 75,000 pamoja na kuchimba mtaro wa urefu wa 10.8 KM na utajumuisha kuunganisha maji majumbani kwa Kaya 50 pamoja na ujenzi wa vituo viwili vya kuchotea maji kwa upande wa Kumuyange.
Kwa upande wa Kigina shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa chanzo, tenki lita 25,000, tenki lita 50,000, tenki lita 120,000 pamoja na ujenzi wa nyumba ya Mitambo (Pump House), Ufungaji wa mfumo wa umeme jua, Ufungaji wa “Pump” ya kusukuma maji, kuchimba mtaro na kulaza bomba 26.6 KM pamoja na kuunganisha maji majumbani kwa kaya 100.
Katika Ziara hiyo Mhe Col Kahabi Mkuu wa Wilaya ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi huo pamoja na kumpongeza Mkandarasi na ameiagiza Ofisi ya Meneja RUWASA kumsimsmia Mkandarasi ili akamilishe utekelezaji wa Mradi huo kwa wakati ili Wananchi wapate kunufaika na mradi huo.
Mhe Col Kahabi Mkuu wa Wilaya ameagiza pia Meneja wa RUWASA kutembelea Kitongoji cha Songambele Kijiji cha Nterungwe ili kutatua changamoto ya ukosefu wa Maji katika Kitongoji hicho.
Kazi inaendelea
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa