- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 30/10/2024,
Mkandarasi Buzubona and Sons Co. Ltd ametambulishwa rasmi kwa Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa Mradi wa maji Kigina na Kumuyange kwa gharama ya Tshs 1,669,188,309.52(bilioni 1.6).
Kulingana na Mkataba Mradi huu unatekelezwa kwa muda wa miezi 6 na unatakiwa kukamilika tarehe 10/03/2025. Shughuli zitakazotekelezwa kwa upande wa Kumuyange ni ujenzi wa chanzo, tenki la Lita 25,000, tenki la Lita 75,000, mtandao wa Bomba 10.8 km na maunganisho ya majumbani kwa Kaya 50.
Kwa upande wa Kigina, Shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa chanzo, tenki Lita 25,000, tenki Lita 50,000, tenki Lita 120,000, nyumba ya mitambo na ufungaji pampu ya Sola, vituo vya kuchotea maji 9, mtandao wa Bomba 26.6km na maunganisho ya maji majumbani kwa Kaya 100.
Kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Ngara, Mhe DC Col Mathias Kahabi, anampongeza sana Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuipata Fedha nyingi Halmashauri ya Wilaya ya Ngara zinazotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo, miradi hii ya Sekta ya Maji
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa