- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkimbia Mbio kutoka Wilaya ya Ngara ameweza kuingia fainali kitaifa katika Mbio Mita 100, na Mita 200. Mashindano Yaliyofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam
Bi Lea ameweza kushika Nafasi ya nne 4 kitaifa katika Mbio za Mita 100 na nafasi ya 6 kitaifa katika Mbio Mita 200.
Mashindano ya Riadha Kwa wanawake ( ladies first) yaliyoandaliwa na Baraza la michezo la Taifa Kwa kushirikiana na Taasisi Toka Japani (JICA).
Lengo la Mshindano hayo ni kupata timu ya taifa Bora ya Riadha Kwa wanawake itakayoshiriki kimataifa.
Nae Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg. Solomon Kimilike amempogeza Bi Lea Kwa kufanya vizuri katika Mashindano ya Riadha Kwa wanawake kwani ameweza kuiwakilisha vizuri Wilaya yetu ya Ngara hususani Mkoa wa Kagera.
Mazoezi ya pamoja kabla ya kuanza Mbio Jijini Dar es salaam
Mkimbiaji Bi Lea akiwa na kiongozi kutoka Ngara Ndg. Bahati Marco.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa