- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ngara Bw. Aidan J. Bahama amewaagiza watendaji wa Kata,vijiji na wenyeviti wa vijiji kuwahimiza wananchi wote juu ya matumizi bora ya vyoo na usafi wa mazingira.
Akizungumza katika kikao cha kupitia takwimu za usafi wa mazingira tarafa ya Nyamiaga, Mkurugenzi alisema kuwa uwepo wa vyoo visivyo bora kuna madhara makubwa sana kwa jamii. Mwananchi mmoja kutokuwa na choo bora anaweza kusababisha magonjwa kwa jamii nzima inayomzunguka,hivyo ni vema wananchi wenyewe kwa wenyewe pia kuhamasishana juu ya faida za kila mwananchi kuwa na choo bora.
Mkurugenzi pia aliwaagiza wataalam wa Afya ya mazingira kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaohatarisha jamii kwa kutokujenga vyoo bora. Mkurugenzi alisema,”Tusiwafurahie wala kuwahendekeza wale wote wanaokaidi kujenga vyoo bora,maana wanatuweka hatarini. Leo tutawachekea ila yakitokea magonjwa ya milipuko itakuwa hasara kwetu sote na si wao peke yao.Hivyo sharia ichukue mkondo dhidi yao”.
Sambamba na hilo,Mkurugenzi aliwaomba wananchi kuwa na umoja ili kwa wale wananchi wasio na uwezo kabisa wa kujenga vyoo bora sababu ya changamoto mbalimbali za msingi kama wasiojiweza,jamii iwasaidie ili kila mmoja kwenye jamii aweze kuwa na choo bora na jamii ibaki salama kwa magonjwa ya milipuko.
Kikao hicho kilifikia maazimio ya kuorodhesha maeneo yasiyofanya vizuri hasa katika usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora ambapo kila msimamizi wa eneo husika anatakiwa kuhakikisha anasimamia usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora na unawaji mikono. Wahusika wa azimio hilo walikuwa Maafisa tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa vijiji,maafisa Afya na WAJA. Pia kikao kiliazimia sheria itumike kwa kuwapiga faini kaya ambazo hazina vyoo bora ili kupunguza kaya zinazopuuzia kuwa na vyoo bora na kutunza mazingira,
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa