- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
27/02/2025
Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Raslimali Watu Bi Jenipha Mapembe amefanya kikao kazi kwa lengo la kukumbushana majukumu mbalimbali ikiwa na mikakati iliyo bora katika kufanya shughuli bora katika Jamii, pia kufahamiana baada ya kuhamia Wilaya ya Ngara.
Kikao hicho wamehudhuria Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa utumishi,Maafisa watendaji kata zote , Watendaji wa Vijiji wote ambao kikao hicho kimefanyika ukumbi wa Community Centre Ngara Mjini.
Nae Afisa Mapato amesisitiza suala la usimamizi wa ukusanyaji Mapato na pasiwe na utoroshaji Mapato katika vijiji/kata . Afisa Elimu Msingi amewataka kusimamia upatikanaji wa chakula shuleni ili kuepusha ufaulu hafifu, Afisa TEHAMA amesisitiza matumizi sahihi ya Mifumo, mitandao ya kijamii pamoja na matumizi bora ya Poss Mashine, Fass na NeST,
Aidha Afisa kilimo amewataka Maafisa Ugani kuwafikia wakulima na wafugaji ,kuwasajili wakulima kwenye mfumo na kupewa namba ya Utambulisho. Afisa Maendeleo ya Jamii amewakumbusha mikopo ya asilimia 10 wahusika ni Vijana, wanawake na wenye ulemavu pia wawapitishie barua za kuomba mikopo kwani ndiyo wanaowatambua waomba mikopo huko kijijini.
Mkuu wa idara ya utawala na usimamizi raslimali watu amesisitiza suala la ushirikiano katika kufanya kazi , pia amewakumbusha majukumu yao maafisa watendaji kata na vijiji, Ujazaji wa PEPMIS, Wajibu na Haki , wafanye Mikutano/ vikao vya kisheria , usomaji mapato na matumizi,kusimamia miradi ya Maendeleo,Suala la Maadili mazuri kazini na nje ya kazi, kuomba ruhusu rasmi anapopata changamoto , kusimamia usafi wa mazingira ,kurudisha vitabu vya Michango na kuacha ulevi kazini.
Ngara kazi inaendelea
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa