- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
Leo 02/2/2025
Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara amefanya Ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Mhe. Col Kahabi alifuatana na Ndg Solomon Kimilike Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya aliyewakilishwa na Mhandisi wa Ujenzi Ndg Simon Mtuka, Wajumbe wa KU Wilaya, Watalaam na wasimamizi wa Miradi ya LADP, Wakandarasi, mafundi ,Pamoja na Wakuu wa Idara toka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Miradi iliyotembelea na Mhe Col Kahabi pamoja na viongozi aliyefuatana nao ikiwa Jumla ni saba kama ifuatavyo;-
1. Ujenzi wa uzio - Kituo cha afya Rusumo - Shs 851m
2. Ujenzi wa Soko la Kimkakati, Kahaza - Shs Bilioni 2.5
3. Ujenzi Rusumo Sec Sch - Shs 260m
4. Ujenzi Ngara High Sch - Shs Bilioni 1.2
5. Ujenzi Lukole High Sch - Shs 260m
6. Ujenzi Shule ya AMALI, Kasharazi - Shs Bilioni 1.6
7. Ujenzi wa Halmashauri HQ - Shs Bilioni 3.5
Miradi yote inaendelea vizuri katika hatua mbalimbali. Aidha, kwa niaba ya wananchi ya Wilaya ya Ngara,
Mhe Col Mathias Kahabi ametoa shukrani nyingi kwa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ambapo miradi mingi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa vema na kwa ufanisi mkubwa.
Mhe Col Kahabi mkuu wa wilaya ya Ngara akiwa kwenye ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo hapa akiwa eneo la soko mkakati la kahaza Rusumo.
Ngara Kazi inaendelea..........
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa