- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa wilaya Mhe. Kanali Mathias Julius Kahabi, ameendelea na ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kata ya Murusagamba vijiji vya Ntanga na Magamba tarehe 13/12/2023.
Mhe Mkuu wa Wilaya akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg. Solomon kimilike, kamati ya Usalama, Wakuu wa Idara na vitengo vya Halmashauri , Viongozi wa Tarura, Nguwasa, Nida, Tanesco pia viongozi wa Kata akiwemo Mhe Diwani wa Kata hiyo.
Hii Ikiwa ni mwendelezo wa Zaira ya oparasheni sikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi Kata Kwa Kata.
Mkuu wa wilaya Mhe kanali.Mathias Julius Kahabi, amewaeleza wananchi namna bora ya kuishi mpakani ambapo aligusia tabia ya wananchi kugawa na kuuza ardhi ya Tanzania kwa raia wa nchi jirani ambapo ametoa onyo kali na katazo la vitendo hivo kukoma mara moja.
Aidha amegusia tabia za wananchi kutoshiriki vikao na kueleza kuwa tabia hiyo ndio chachu ya migogoro mingi ndani ya kijiji na kuwashauri kuwa na umoja, upendo na mshikamano pamoja na kuweka uzalendo mbele ili vijiji vyetu vipate maendeleo na Taifa kwa ujumla.
Pia Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg.Solomon Kimilike aliwaasa wananchi kuwa wazalendo na kuwa na umoja.
Mkurugenzi Mtendaji Mtendaji ameunda kamati ya muda ya kufatilia baadhi ya changamoto zilizobainika katika kijiji cha Murugunga na kutoa maelekezo juu ya kamati hiyo kuanza kazi mara moja ili kupata suluhisho la changamoto zote zilizobainika huku baadhi zikiwa zimetatuliwa hapo hapo na viongozi waliopewa nafasi ya kujibu kero hizo.
Diwani wa Kata hiyo Mhe Sudi Mkubila alipongeza Mhe Mkuu wa wilaya na timu yake Kwa kuanzisha zoezi la kusikiliza na kutatua kero Kwa wananchi Kata Kwa Kata.
Mkuu wa wilaya ya Ngara akiongea na wananchi wa Kata ya Murusagamba walayani Ngara katika zoezi la oparasheni tatua kero.
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg. Solomon Kimilike wa kwanza kulia akiwa na Wakuu wa Idara katika zoezi la oparesheni tatua kero Kata ya Murusagamba.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa