• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

NAIBU WAZIRI DKT. KIRUSWA AUTAKA UONGOZI WA MGODI WA TEMBO NICKEL KUANDAA MPANGO WA ENEO LAO

Wakati ilipowekwa: September 23rd, 2023

Asema Rais Samia anatamani kuona utekelezaji wa mradi huo uendelee kwa kasi ili kutimiza lengo la kuanzishwa

Ataka Mradi huo kuwa wa mfano kupitia mpangokazi kuepuka migogoro

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa  ameutaka Uongozi wa Mgodi wa Tembo Nickel kuandaa na kuwasilisha Serikalini Mpango Mkakati unaoonyesha namna wanavyoenda kushughulikia eneo lote la leseni ili kuhakikisha wanaepuka migogoro na wananchi wanaozunguka eneo hilo.

Alisema hayo Septemba 20, 2023 wakati akizungumza na uongozi wa mradi wa Tembo Nickel unaomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Kabanga Nickel, uliopo Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za Sekta ya Madini katika Mikoa ya Kagera na Geita. 

“Mradi huu tunataka uwe wa mfano hapa nchini, hatutaki kurudia makosa yaliyotokea huko nyuma kutokana na miradi kuingia kwenye migogoro na wananchi wanaozunguka maeneo yao, nyie muwe mfano katika kuepuka hili kupitia mpango kazi wenu” alisema Dkt. Kiruswa.

Aliwataka kuratibu suala la kuwalipa fidia na kuwahamisha wananchi ili kuepuka usumbufu na kwamba wahakikishe wanawalipa fidia kwa awamu ili kusiwe na usumbufu wakati bado hawajahamia katika nyumba wanazojengewa, ili kila mguswa ahamie kwenye nyumba yake akiwa na fedha za kujikimu na kuendeleza maisha yake.

“Tunaomba mkamilishe haraka utaratibu wa malipo ya fidia na yaende sambamba na uhamishaji wa wananchi na mlete hizo taarifa wizarani. Pia tunataka tujue ujenzi wa hizo nyumba unaanza lini na unaisha lini” alisema Dkt. Kiruswa. 

Alisema kuwa Rais Samia anatamani kuona utekelezaji wa mradi huo ukiendelea kwa kasi ili kutimiza lengo la kuanzishwa kwake, kwakuwa mgodi huo unazalisha miongoni mwa  madini ya kimkakati ambayo kwasasa mahitaji yake ni makubwa duniani.

Aliutaka mgodi huo kupeleka huduma zote muhimu kama shule, barabara na   maji,  katika maeneo utakaohamishia watu ili wapate huduma zote muhimu kwani ni haki za msingi.

 www.ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • DC NGARA MHE COL MATHIAS KAHABI AKUTANA NA BRIG GEN GABRIEL E. KWILIGWA - KAMANDA BRIGDE YA MAGHARIBI.

    May 16, 2025
  • MHE COL MATHIAS JULIUS KAHABI DC NGARA ASHIRIKI USAFI NA WANANCHI WA NAKATUNGA

    May 15, 2025
  • MWENYEKITI WA CCM AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO - NGARA

    May 16, 2025
  • KIKAO KAZI CHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AFUA ZA LISHE WA KILIMO CHA MAHINDI CHAFANYIKA - NGARA

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa