- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara, leo tarehe 12/12/2024, akifuatana na KU Wilaya, Afisa Tarafa Murusagamba, Diwani Kata ya Muganza pamoja na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wa Kata ya Muganza amefunga rasmi mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba(Mgambo) yaliyokuwa yakiendeshwa katika Tarafa ya Murusagamba, Kata ya Muganza, Kijiji cha Muganza.
Jumla ya wahitimu 76 wamemaliza mafunzo hayo, kati yao wahitimu 74 ni wanaume na 2 ni wanawake. Mafunzo hayo yalifunguliwa tarehe 03/6/2024 yakiwa na jumla ya wanafunzi 127 lakini kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro na baadhi kushindwa kumudu mafunzo hayo hawakuweza kumaliza.
Mhe Col Mathias Kahabi, amewapongeza wanafunzi, wakufunzi na wananchi wa Kata ya Muganza kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha toka mwanzo wa mafunzo hadi kuhitimishwa kwake. Aidha, amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kwenda kuishi Kiapo chao cha utii kwa Mhe Rais na Amiri Jeshi Mkuu pamoja na kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Tanzania.
Amewakumbusha kwamba Wilaya ya Ngara iko mpakani na inapakana na nchi mbili za Burundi na Rwanda hivyo lazina kudumisha mahusiano mema yaliyopo na jirani zetu lakini pia kuhakikisha wanasaidiana na Idara ya Uhamiaji pamoja na Vyombo vingine vya Usalama kudhibiti Uhamiaji haramu kwa kutoa taarifa pindi kunapotokea wachache kuingia nchini kinyume na taratibu na sheria za nchi.
Mhe Col Mathias Kahabi DC Ngara, pia amewasisitiza wahitimu kwenda kushirikiana na Jeshi la Polisi katika ulinzi wa raia na mali zao kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
Ss
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa