- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
19/12/2024
Katika Mashindano ya Tamasha la utamaduni Mkoa wa kagera lililoandaliwa na Mhe Hajat Fatma Mwasa Mkuu wa mkoa wa kagera na kushirikisha Halmashauri /wilaya za mkoa wa kagera.
Tamasha hilo lililoshirikisha Mashindano ya Vazi la asili, ngoma na maonesho vitu asili.
Halmashauri ya Ngara imeweza kushika nafasi ya 1 kimkoa katika shindano la Mavazi ya asili.Ambapo matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
1. Ngara - 94
2. Biharamulo - 88
3. Bukoba MC - 87
4. Kyerwa - 83
5. Missenyi - 75
6. Karagwe - 68
7. Muleba - 66
8. Bukoba DC - hawakushiriki
Mshindi wa kwanza amepata tsh 300,000/ na cheti, Mshindi wa pili tsh 200,000/ na cheti na Mshindi wa tatu tsh 100,000/na cheti.
Katika Ngoma za asili matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
1 Bukoba manispaa 82.5
2 karagwe 78.5
3 Muleba 70.75
4 Ngara 68.4
5 kyerwa 66.5
6 Biharamulo 66.4
7 Misenyi 62.6
8.Bukoba Dc 27.3
Mshindi wa Ngoma wa kwanza tsh 300,000 na cheti, mshindi wa pili tsh 200 000 na cheti ,mshindi wa tatu tsh 100,000 na cheti
Zawadi hizo zimetolewa uwanja wa kaitaba Bukoba ambapo Tamasha hilo limefanyika.
Mgeni rasmi katika Tamasha la utamaduni.mkoa wa kagera ,liliohusisha mambo mbalilimbali ikiwemo.uwekezaji kagera na maonesho mbalimbali alikuwa Mhe Dkt Doto Mashaka Biteko Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati.
Tamasha hilo limehudhuliwa na mhe Inocenty Bashungwa waziri wa mambo ya ndani ,viongozi wa mkoa , wakuu wa wilaya, wenyeviti wa Halmashauri ,meya manspaa, wakurugenzi watendaji, makatibu tawala wilaya, na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali kutoka kila hamashauri ya wilaya.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa