- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wazazi wote katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuhakikisha wanaongeza miundombinu katika shule za msingi na za sekondari, ili waweze kukidhi ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na masomo kila mwaka.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Gideon Samson Mwesiga Januari 15, 2019, kwamba uzoefu umeonyesha kila mwaka wanafunzi wanaojiunga darasa awali, la kwanza na kidato cha kwanza wanaongezeka mara dufu.
“Tumejifunza kwamba kadili tunavyoandikisha watoto kila mwaka; ndivyo tunavyopata wanafunzi wengi zaidi na ndivyo mahitaji ya miundombinu yanavyoongezeka, kwa hiyo wazazi wote wanawajibika kuandaa miundombinu hiyo, kusudi tuweze kuwasaidia watoto wetu.” Alisema Ndugu Mwesiga.
Amesema wamejifunza kwamba mpango wa serikali wa elimu bila malipo, limesababisha ongezeko kubwa la wanafunzi katika shule za sekondari na zile za msingi kila mwaka; huku akiongeza kwamba mwaka 2019 tunatarajia kusajili wanafunzi wapatao 21,000 kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na awali.
“Wito wangu kwa wananchi tujitahidi kuweka benki ya matofali, mawe na mchanga na halmashauri itaweza kutoa vifaaa vya viwandani, ili tujenge miundombinu kwa ajili ya kuwawezesha watoto wetu kujifunza bila bughudha.” Alishauri Ndugu Mwesiga.
Pia aliwasisitiza wazazi kuwahimiza wanafunzi wahudhulie masomo yao kama taratibu na kanuni za serikali zinavyowataka; huku akiwataka wazazi hao wahakikishe watoto wao kuwapa mahitaji muhimu ili waweze kuyamudu masomo yao.
Akiongelea changamoto, amesema kufikia Desemba 2018; idara ya elimu msingi ilikuwa ina mahitaji ya vyumba vya madarasa vipatavyo 1869; lakini ina upungufu wa vyumba 1059, nyumba za walimu 1207, matundu ya vyoo yapatayo 775, ambapo mapungufu ya ofisi za walimu ni 251.
Hata hivyo, amesema idara ya elimu msingi ina mapango wa kutumia mapato ya ndani, kugharimia vifaa vya viwandani, kwa ajili ya kusapoti nguvu za wananchi, ili kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa madarasa.
Pia, idara kwa kushirikiana na Mh. Mbunge wa Jimbo la uchaguzi la Ngara, watachangia ujenzi wa miundombinu kupitia mfuko wa jimbo; pamoja na kuendelea kuweka kwenye bajeti maombi ya fedha za ujenzi wa miundombinu hiyo.
Aidha, amesema kupitia mradi wa Local Area Development Program (LADP) Halmashauri itajenga vyumba vya madarasa 10, majengo ya utawala 02, nyumba za walimu 02, matundu ya vyoo 24, pamoja kutengeneza madawati na viti ingawa idfadi kamili haijajulikana katika shule za Mgoma na Mkugwa.
Ameishukuru serikali kwa jitihada inazozifanya kwani tangu Julai hadi Novemba 2018 idara ya elimu msingi, imepokea shilingi 316, 426,000.00 kwa ajili ya elimu bila malipo; rusuku ya uendeshaji wa shule 173,926,000.00; posho ya madaraka kwa walimu wakuu 115,000,000.00 pamoja na 27,500,000.00 kwa ajili ya posho ya maafisaelimu kata.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa