- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa Kagera Hajat Fatma Mwassa amewapongeza Madaktari pamoja na Wauguzi wa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba jinsi wanavyoendelea kutoa huduma bora na nzuri kwa watoto wachanga wanaozaliwa hospitalini hapo.
Pongezi hizo amezitoa leo Disemba 15, 2024 alipofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba akiambatana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kuwajulia hali pacha wanne (4) waliozaliwa hospitalini hapo mnamo tarehe 29.11.2024, wanaoendelea kupatiwa huduma pamoja na uangalizi hopitalini hapo.
Aidha Mhe. Fatma Amesema kuwa, Serikali ya Mkoa Kagera kupitia Ofisi ya Mganga Mkuu wataendelea kuwaangalia kwa ukaribu zaidi watoto hao pamoja na Watoto wengine waliozaliwa kabla ya muda (Watoto Njiti) pamoja na wenye changamoto ili waweze kuwa na afya njema.
Sambamba na hilo, Hajat Mwassa ametoa zawadi mbalimbali kwa pacha hao huku akitoa pongezi kwa wazazi wa watoto hao kwa kupata zawaidi pacha wanne.
Naye baba mzazi wa pacha hao Benson Eustace ambaye ni Mwandishi wa habari wa Azam TV amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa kwa kufika hospitalini hapo kwaajil8 ya kuwajulia hali watoto wake huku akitoa pongezi nyingi kwa Uongozi, Madaktari pamoja wauguzi wa Idara ya Watoto Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba kwa huduma nzuri pamoja na ushirikiano wao katika kuwahudumia watowo hao.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa