- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
15/09/2025
Mhe Col.Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara ametoa salam za Pongezi na Shukrani kwa viongozi na Wananchi kwa Mapokezi, Hamasa kubwa kwenye miradi , Mkesha na kuukabidhi Wiliya ya Biharamulo.
Mhe amemshukuru na kumpongeza Ndg Solomon kimilike Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya Ngara kwa ushirikiano mkubwa aliyoutoa pia Mwl. Said Salum Mratibu wa Mwenge na wasaidizi wake kwa usimamizi , na kuwa kiungo kwa kamati mbalimbali aidha 6amewashukuru kamati ya Usalama wilaya na walio chini yako kwa ushirikiano mkubwa.
Mhe Col. Kahabi aliendelea kuwashukuru wakuu wa idara na vitengo H/ Wilaya , kamati zote za maandalizi, kamati ya siasa chama cha mapinduzi ikiongozwa na comred Vitalis Ndailagije, viongozi wote wa Madhehebu ya Dini, Wakuu wa Taasisi za Serikali, Maafisa Tarafa,viongozi wa vyama vya siasa,Wakuu wa Taasisi Binafsi , Mashirika na Makampuni ,Maafisa watendaji kata na vijiji,Watendaji wa Mamlaka za Ngara Mjini na Rulenge, Maafisa Elimu kata, Maafisa kilimo kata ,Maafisa Mifugo kata ,Maafisa Maendendeleo ya kata, Maafisa afya kata, wakuu wa shule za Sekondari za Serikali na Binafsi , walimu wakuu wa shule za msingi za serikali na Binafsi,wasimamizi wa miradi , Chief Nsoro na chief Baramba, Wafanyabiashara na wajasiliamali ,Wakulima na wafugaji,Watumishi wote wa umma,Vijana wa Hamasa,Vijana wa Halaiki,Vijana wa kongamano,wasanii mbalimbali,Waandishi wa Habari ,Vijana wa Skauti,Wanafunzi wote , Madereva na wananchi wote waliohudhuria.
Aidha Mhe Col . Kahabi amewashukuru watu wote kwa kufanikisha shughuli za Mwenge wilayani Ngara, pia ameendelea kwa kusema Ahsnteni sana anawashukuru na kuwapongeza kwa kujitolea kwa hali na mali,
"Jitokeze kushiriki Uchaguzi mkuu October 29/2025 kwa aman na utulivu"
Ngara kazi inaendelea
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa