- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe Col Mathias Julius Kahabi - DC Ngara kwa niaba ya Kamati ya Ulinzi na Usalama (KU) Wilaya anawatakia Heri ya Mwaka MPYA 2025 Wananchi wote wa Wilaya ya NGARA washerehekee kwa amani na utulivu kwani Vyombo vya Usalama vimejipanga vema kuhakikisha sherehe hizi zinamalizika salama.
Aidha, Jeshi la Polisi litaimarisha hali ya Ulinzi na Usalama katika maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya hususan maeneo yote ya Mikesha ya Mwaka Mpya ikiwemo Makanisani pamoja na Kumbi za starehe na burudani.
Mhe Col Mathias Kahabi anawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kipindi chote cha Sherehe za Mwka MPYA kwa kutoa taarifa za matukio yasiyokuwa ya kawaida na yanayoweza kuhatarisha Usalama wa raia na mali zao wakati wa sherehe.
Aidha, wananchi wanashauriwa kuzingatia maagizo/maelekezo yafuatayo wakati wote wa sherehe za Mwaka MPYA;-
1. Watoto muda wote katika matembezi yao wakati wa Sikukuu wafuatane na mtu mzima/mzazi/mlezi ambaye atahusika kulinda Usalama wao.
2. Vijana wa boda boda wajiepusha na uendeshaji wa pikipiki usiozingatia Sheria za Usalama barabarani.
3. Uchomaji wa matairi kama ishara ya kuuona Mwaka Mpya ni marufuku.
4. Fujo/kupigana/vurugu kwenye Kumbi za starehe ni marufuku.
5. Kila mwananchi awe mlinzi namba moja wa usalama wake na wa mwenzake pia pamoja na mali yake.
6. Polisi muda wote wataimarisha doria hivyo wananchi wasiwe na hofu na uwepo wao mitaani kwani ni sehemu ya majukumu yao.
7. Aidha, wananchi toeni ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Polisi pindi inapohitajika ili sherehe za Mwaka MPYA 2025 zimalizike kwa amani na salama.
Kwa mara nyingine tena Mhe Col Mathias Julius Kahabi anawatakia Wananchi wote wa Wilaya ya Ngara Heri ya Mwaka Mpya 2025.
Ngara Kazi inaendelea..
Ahsanteni sana - Mulakoze Cyane.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa