- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Salamu nyingi za shukrani natoa kwenu wana Mbeya, mikoa ya jirani na wote mliotoa muda wenu kuhudhuria sherehe za kilele za Mbio za Mwenge wa Uhuru. Na kubwa zaidi ni Uzinduzi wa Kitabu cha kumbukumbu ya Miaka 60 ya Mwenge wa Uhuru.
Mwenge wa Uhuru 2025 umeacha historia kubwa sana. Ukiacha umbali uliokimbia na idadi ya miradi iliyokaguliwa na thamani yake ni wazi kuwa Mbio za Mwenge mwaka huu zimeacha historia katika masikio na macho yetu kutokana na ukweli kuwa sherehe zimepambwa vzr na halaiki ya safari hii ilikuwa ya kipekee na yenye kusisimua.
Hii inatokana na ainaya watu walioshiriki ambapo kwa mara ya kwanza Watoto wenye Ulemavu wa viungo nao pia wameshiriki. Ni jambo ambalo halijawahi tokea.
Kama ilivyoada Kilele uanza na misa takatifu ya kumuombea Baba wa Taifa , Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Tunalishukuru Kanisa katoliki kwa kuongoza misa hiyo kwa mafanikio makubwa. Tuzidi kumuombea Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Mgeni Rasmi Dr. Philip Mpango , Makamu wa Rais Wa JMT alifunga maonyesho ya kazi za vijana yaliyofanyika kwa siku 7 katika eneo la uhindini hapo hapo Mbeya. Maonyesho haya yalionyesha vipaji mbalimbali vya vijana na ubunifu. Nayo yameacha kumbukumbu nzuri kwa idadi ya washiriki na kazi walizoshiriki. Kwa hakika imefana sana.
Mwenge wa Uhuru 2026 unataraji kuwashwa Mkoa wa Kusini Pemba na baada ya kuzungushwa Nchi nzima utafikia kilele Mkoani Rukwa ambapo pia tutafanya Maonyesho ya kazi za Vijana katika wiki ya vijana, pamoja na kongamano kubwa la Vijana.
Ninarudia kuwashukuru sana Wanambeya kwa ushiriki na utayari wao. Kipindi chote umeonyesha utayari kwa kuhudhuria kwa wingi wiki ya maonyesho ya kazi za vijana. Kila siku makundi kwa makundi; ushiriki wenu kwenye Kongamano la Vijana na uwazi wetu katika kujadili na wisho ushiriki wenu kwenye misa. Tunawashukuru sana. Kwa hakika wameuenzi Mwenge wa Uhuru ambao umeendelea kuwa moja ya Tunu katika Umoja wa Nchi yetu.
Asanteni Mbeya
#MwengeWaUhuru2025
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa