- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali imeelekeza Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Barabara ya Lusahunga-Rusumo kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kuleta tija kwa wananchi na watumiaji wa eneo hilo. Mradi huo, wenye thamani ya shilingi bilioni 153, unatekelezwa na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC), chini ya usimamizi wa makampuni ya Noplan na Tisa.
Ujenzi wa barabara ya Lusahunga-Rusumo kwa kiwango cha lami, inayounganisha Tanzania na nchi jirani za Rwanda, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, unatarajiwa kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta ya usafirishaji.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, alibainisha hayo alipokagua maendeleo ya mradi huo. Alisema barabara hii ni kiunganishi muhimu kwa Tanzania na nchi jirani, kwani inatumika kusafirisha mizigo kutoka bandarini, hali itakayochochea uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya wananchi.
Hata hivyo, Naibu waziri kasekenya aliwataka wasimamizi na wakandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo, ambao upo nyuma kwa asilimia 18. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha mradi unakamilika kwa viwango vya juu ili kuendana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.
Kwa upande wake, Msimamizi wa Mradi,Mhandisi George Mwandiga, alisema barabara hiyo itakuwa na urefu wa kilomita 92 na kujumuisha madaraja na makaravati 133. Mradi huo unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 153, fedha zinazotolewa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.
Mmoja wa wananchi wanaotumia barabara hiyo, Mussa Abeli Kaleji, ameishukuru serikali kwa hatua hiyo. Pia, amempongeza mkandarasi wa mradi kwa kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo hatua inayochangia kuboresha maisha yao.
Utekelezaji wa mradi ulianza rasmi tarehe 5 Julai 2024, na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 5 Julai 2025. Hadi sasa, kazi za ujenzi zimefikia asilimia 20 ya utekelezaji wake. Serikali imesisitiza umuhimu wa kasi ya utekelezaji kuongezwa ili kuhakikisha lengo la mradi linafikiwa kwa wakati uliopangwa.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa