- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Leo imefanyika hafla fupi ya ugawaji wa Mipira ambayo imetolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) kupitia programu ya Football for schools (F4S) Ikiwa ni jitihada za Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza michezo nchini Tanzania kwani amekuwa mstari wa mbele kuendeleza na kukuza sekta ya kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri katika michezo ya Ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Hafla hiyo imeongozwa na Mhe Sunday Mukozi aliyemuwakilishwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Wilbard Bambara ambapo kila shule imepatiwa Mipira kumi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na kaimu Afisa Elimu Mwl. Ezekiely Zabayanga, Maafisa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Maafisa Elimu Kata, Walimu Wakuu, Walimu wa Michezo na wanafunzi wanamichezo ambapo hafla hiyo imefanyika Ukumbi wa TRC Ngara Mjini.
Picha ya pamoja Mgeni Rasmi, kaimu Afisa Elimu Mwl. Ezekiely Zabayanga, Maafisa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Maafisa Elimu Kata, walimu Wakuu , walimu wa Michezo na wanafunzi wa michezo.
Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi, Maafisa Utamaduni Sanaa na Michezo, Maafisa Elimu Kata, walimu Wakuu na Walimu wa Michezo.
Mhe. Sunday Mukozi akigawa Mipira kwenye hafla.
Afisa utamaduni Wilaya ya Ngara Mhe. Said Salum akiongea kwenye hafla fupi ya ugawaji wa Mipira.
Kaimu Afisa Elimu Mwl. Ezekiely Zabayanga akiongea kwenye hafla hiyo.
Mhe. Sunday Mukozi aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Wilbard Bambara akiongea kwenye hafla hiyo fupi.
Mwalimu baada ya kupokea Mipira Kutoka Kwa Mgeni Rasmi.
Walimu wa shule za Msingi wakiwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa