- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Nchi Tatu Wanachama wa Mradi wa Umeme kupitia Baraza la Mawaziri wa masuala ya Nishati kutoka Tanzania, Rwanda na Burundi tayari zimekubaliana kuzindua Mradi wa Umeme wa Rusumo HydroPower Project ifikapo Februari 2025 hii ni kutokana na ratiba za Wakuu wa Nchi hizo.
Akizungumza na Wanahabari mara baada ya kuhitimisha Kikao cha makubaliano, kilichofanyika Rusumo Wilayani Ngara mahala unapotekelezwa mradi huo, Mwenyekiti wa Baraza hilo la Mawaziri ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Dotto Mashaka Biteko, amesema mpaka sasa mradi umekamilika 99.9% kinachosubiriwa ni ratiba ya Wakuu wa Nchi zote Tatu ambao wamekuwa na majukumu na ratiba ikishindikana kuwapata kwa pamoja, ili kufanyika kaa tukio la uzinduzi rasmi wa Mradi huo wa megawati 80.
Aidha Dkt. Biteko amezishukuru Nchi wanachama kwa namna walivyoshirikiana katika utekelezaji wa mradi huo, huku akitaja manufaa makubwa yaliyopatikana kwa Wananchi wanaouzunguka mradi huo, yakiwemo upatikanaji wa Umeme wa uhakika, Ajira kwa Wafanyakazi na Vibarua wakati wa utekelezaji wa mradi, ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotokana na mradi hususani Wilayani Ngara ikiwemo Hospitali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kagera Amesema kuwa, kwa sasa Mkoa wa Kagera hautakuwa na katizo la Umeme, kwakuwa umeme utakaozalishwa wa Megawati 27 utaunganishwa moja kwa moja katika gridi ya Taifa, hivyo umeme utaimarika, na kuwaomba wawekezaji kuendelea kuwekeza katika Mkoa Kagera kwa kujenga Viwanda na kuongeza shughuli nyingine za uzalishaji kwani tayari nishati ya umeme ni ya uhakika.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa