• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

Tokomezeni Udumavu wa Watoto: Mwesiga

Wakati ilipowekwa: October 10th, 2018

Kamati ya lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, imetakiwa kuhakikisha inatekeleza shughuli za kutokomeza udumavu wa watoto, kama ilivyoainishwa katika mkataba wa mradi wa Mtoto Mwerevu.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Gideon Samson Mwesiga, ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya lishe, kilichofanyika Oktoba 10. 2018 katika ukumbi wa Halmashauri.

“Kamati ya lishe ya wilaya ihakikishe inasimamia na kutekeleza majukumu yake ya kupunguza udumavu kila mjumbe kutambua majukumu yake hasa kuielimisha jamii itambue athari za udumavu na jinsi ya kuutokomeza.” Alisema Mwesiga.

Amewataka wajumbe wa kikao hicho kujadili shughuli za lishe, zilizofanyika katika kipindi cha Julai - Septemba 2018, ili kuhakikisha jamii inapata elimu sahihi katika suala zima la lishe bora kwa watoto.

Wakati huo huo, Mratibu wa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu John Sosthenes amesema kupitia Mradi wa Mtoto Mwerevu  kwa kutumia watoa huduma ngazi ya jamii (WAJA) wajawazito na watoto chini ya miaka miwili wamepata elimu ya kubadili tabia ya masuala ya lishe bora.

Amesema tabia hizo zimegawanyika katika makundi tofauti ambapo ya kwanza inajumuisha umuhimu wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi 6, bila mtoto kupewa chakula chochote hata maji.

Amesema kwamba baada ya miezi 6 mtoto apewe chakula cha nyongeza chenye virutubishi vyote muhimu; huku akiitaja tabia ya tatu kuwa ni usafi wa mazingira, na tabia ya nne ni ushiriki wa akina baba katika malezi na makuzi ya mtoto.

Alisisitiza kwamba katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2018, licha ya kuwa na changamoto ya kutopata fedha kwa wakati, wamefanikiwa kufanya usimamizi elekezi kwa WAJA, juu ya utoaji elimu sahihi kwa walengwa wa mradi wa mtoto mwerevu.

Aidha, wamefanikiwa kutoa matone ya vitamin A kwa watoto wa miezi 6-59, utoaji wa madini chuma kwa wakina mama wajawazito, unyonyeshaji maziwa ya mama pekee kwa watoto (EBF) na akina mama wenye watoto miezi 0-23.

Kikao hicho kiliwasilisha shughuli za utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha julai hadi septemba 2018, na kujadili taarifa za utekelezaji wa shuguhuli za lishe katika kipindi cha miezi mitatu, na kutambulisha shughuli ya kutokomeza utapiamlo (Positive Deviance Hearth).

Matangazo

  • TANGAZO LA TATHMINI YA UJUZI NA UZOEFU KATIKA WILAYA YA NGARA KUTOKA TEMBO NICKEL August 30, 2022
  • MREJESHO WA MPANGO NA BAJETI YA HALMASHAURI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023 KWA KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO TAREHE 12 AGOSTI, 2022 September 23, 2022
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2022 HALMASHAURI YA WILAYA YA NGARA December 04, 2022
  • RIPOTI YA ATHARI ZA KIMAZINGIRA NA KIJAMII MRADI WA MAEGESHO YA MAGARI BENAKO December 01, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • NGARA FAMERS YATOA KATONI ZA BISCUIT.

    December 07, 2023
  • NGARA OIL YATOA KATONI ZA MAJI NA JUICE KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA UHURU WA TANZANIA BARA KIWILAYA.

    December 06, 2023
  • CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA NGARA CHATOA KATONI ZA MAJI NA JUICE KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU KI-WILAYA.

    December 06, 2023
  • RATIBA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 62 YA UHURU WA TANZANIA BARA WILAYANI NGARA KUANZIA TAREHE 04/12/2023 HADI 11/12/2023

    December 13, 2023
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa