- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kutumia muda wao kufanya toba, kumshukuru Mwenyezi Mungu pamoja na kuishi vizuri na watu wenzao, huku akiwataka kuacha mambo mengine kwa Mungu.
Hayo ni kwa mujibu wa Mchungaji wa Kanisa la Kiluteli la Kikiristo Tanzania Oscar Samwel, wakati wa ibada ya kumuaga aliyekuwa Afisaelimu idara ya sekondari Marehemu Fikeni Ezekiel Senzighe, iliyofanyika katika Kanisa la Kiluteli Wilayani Ngara Mei 01, 2019.
“Kila mtu ajiadae nafsi yake ili siku mwili ukifa, roho zettu zikapate kibali mbele ya Mungu, mwenzetu ameotangulia, sisi tumshukuru Mungu hata kwa muda mfupi alioishi Ngara.” Alkisema Mchungaji Samwel.
Ameonya kutoyafanyia kazi maswali yanayoweza kujitokeza, kwa sababu ya ubinadamu wetu; kwa kudai kwamba hakuna hata mmoja mwenye majibu sahihi ya maswali hayo, na hata majibu yakiwepo hakuna la kufanya.
Ameyataja maswali hayo; kwanini amekufa wakati kakaa muda mfupi katika ofisi hiyo? alipata ajali juzi, kwa nini kafa kwa ajali kama ile? mbona na dereva waliyekuwa naye alikuwa amepata ajali hivi karibu? na mbona aliyemtangulia katika nafasi hiyo naye alikufa kwa ajali?
Kadiri ya Mchungaji Samwel maswali hayo yakipewa nafasi yataleta uhasama, chuki na kusababisha watu wakosane bure, wakati inafahamika kuwa maisha ya binadamu hapa duniani si ya kudumu, huku akisisitiza kwamba kila nafsi itaonja mauti.
“Nawakubusha imeandikwa kwamba kila nafsi itaonja mauti; iwe kwa ajali, kuuawa kwa sumu, kukatwakatwa panga, na hata kwa kuugua, bado ni kifo tu; tunalopaswa kufanya ni kujipatanisha na Mungu pamoja na wenzetu.” Alisema mchungaji Samwel.
Aidha, Afisaelimu Mkoani Kagera Ndugu Aloyse Kamamba, amesema marehemu alikaa muda mfupi katika idara ya elimu sekondari, lakini alikuwa msaada sana kwake; kwani walikuwa wakifanya naye kazi kwa karibu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, ameushukuru uongozi wa wilaya ya Ngara, kwa ushirikiano walionyesha tangu kutokea kwa ajali hadi mauti ya mwenzetu, na kuwataka wahudumishe ushirikiano huo.
Marehemu Senzighe alifariki dunia na wenigne watano kujaruhiwa April 30, 2019, katika pori la Kimisi Wilayani Karagwe mkoani Kagera, baada ya gari aina ya Landcruser lenye usajili wa Namba STK 6591 kupinduka.
Kamanda Malima amemtaja dereva wa gari hilo kuwa ni Ndugu Stanley, ambapo majeruhi wa ajali hiyo ni Askari Amenya Nestory, aliyepewa rufaha kwa ajili ya matibabu zaidi April 30, 2019 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza.
Wahanga wengine wa ajali hiyo ni Afisaelimu Vifaa na Takwimu Ndugu Martoni James, Afisaelimu Taaluma Ndugu Gerad Nyahonge pamoja na Jebili Abdallah ambaye ni askair polisi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa