- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Tusimamie taratibu za vyama vya ushirika, ili imani ya wananchi kwa vyama vyetu vya ushirika irejee waweze kuweka hisa zao; hakuna njia ya mkato, lazima vyama hivi viwe na nguvu.” Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elias Gaguti alitoa wito huo kwa Viongozi wa Wilaya ya Ngara.
Brigedia Jenerali Gaguti alitoa rai hiyo Septemba 08, 2018, wakati wa ziara yake ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, ikilenga kuutambua mkoa wa Kagera, ili kwa pamoja waweze kupanga watavyowatumikia wananchi.
Akijibu taarifa, Brigedia Jenerali Gaguti amesema amegundua changamoto kubwa, iko katika suala la kahawa baada ya maelekezo ya awali ya serikali, na akakiri kwamba kazi kubwa ya kukusanya kahawa, kutoka kwenye vyama vya msingi kwenda kwenye vyama vikuu, imekwishafanyika na inaedelea kufanyika.
“Langu katika hili, nataka twende pamoja kama kama mkoa tubaki kwenye msingi, ambao umetolewa maelekezo na serikali, kwamba lazima kahawa ikusanywe kupitia vyama vya msingi kwenda vyama vikuu, kwa ajili ya kupelekwa sokoni licha ya changamoto zilizopo.” Alisema Brigedia Jenerali Gaguti.
Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera amewataka viongozi waendelee kuwatia moyo wakulima, kwa kuwaeleza kwamba tatizo la ukusanyaji kahawa, serikali inalitambua na italitolea maelekezo ya ziada, ili kuwaondolea wananchi wasiwasi.
Ameutaka uongozi wa wilaya ya Ngara na wa mkoa kuvisimamia vyama vya ushirika, akidai kwamba hakuna njia ya mkato katika hilo; vyama vya ushirika ni lazima viendelee kufanyakazi iliyokusudiwa.
“Tumeanza na changamoto nyingi, lakani natumaini huko mbele ni pazuri, hata hivyo hili ni somo kwetu; ukiangalia vyama vya ushirika hasa kwa upande wa korosho, vimefanikiwa sana lakini hawakuanza kwa mafanikio ya asilimia 100.” Alisema Brigedia Jenerali Gaguti.
Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kwamba imani yao kwa vyama vya ushirika inarejeshwa kwani wakulima wamekosa imani na vyama hivyo; kwa hiyo, lazima vijipange kurejesha imani hiyo kwa wakulima na wanachama wao; wilaya na mkoa wana dhamana kubwa ya kusimamia hilo.
Wakati huo huo, amefurahishwa na utendajikazi wa kiwanda cha kahawa cha Ngara Coffee, baada ya kuona mashine za kukoboa kahawa na kahawa iliyokuwa imekoborewa iko tayari kupelekwa sokoni.
“Ofisi yangu iko wazi pale mtakapohitaji ushauri na maoni kutoka kwetu, tunakuhakikishia kwamba utapata msaada wetu, hatutakukwamisha, mradi tu tuwe na uwezo wa kutatua tatizo lako.” Alisema Brigedia Jenerali Gaguti.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa