- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
11/03/2025
Kamati ya fedha utawala na Mipango imetembelea kuona ukamilishaji wa ujenzi wa soko hilo utagharimu Tsh 2,517,833,024/= na ambao umefikia asilimia 93.90
Makamu Mkiti wa Halmashauri Mhe Adronizi Bulindori aliongozana na kamati ya fedha ambao ni waheshimiwa Madiwani wajumbe wa kamati hiyo wakuu wa idara na Vitengo pamoja na Mratibu wa LADP Ndg Asifiwe Gwihangwe.
Mradi huo una sehemu kuu sita ambazo ni Eneo la wazi kwa ajili ya Biashara za jumla na rejareja,Sehemu za kuhifadhi Bidhaa,Maduka na maeneo ya wazi kwa ajili ya ofisi mbalimbali , eneo la maegesho ya magari na Eneo la Minada
Faida za mradi ikiwa ni
Kuongeza mapato ya Halmashauri ambapo itakusanya mapato kutokana na ushuru wa kupakia na kupakua mizigo,kodi za vibanda,ofisi na ushuru wa maegesho.
Kuboresha mahusiano na nchi jirani baina ya Tanzania na Rwanda
Fursa za Ajira yaani katika utekelezaji wa mradi huu watanzania mbalimbali hasa wakazi wa Ngara ameajiriwa kwa muda mfupi ,kati na mrefu.
Kuinua kipato cha wananchi kupitia mradi huu wananchi wengi hasa wa wilaya ya Ngara wamenufaika hasa kupitia kutoa huduma na kuuza bidhaa mbalimbali kama vifaa vya ujenzi, vyakula,nyumba za kupanga na bidhaa nyingine zinazohitajika wakati wa utekelezaji mradi huo.
Kukuza mji wa Rusumo kwani mradi huu utakuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa mji wa Rusumo hasa kutokana na kuongezeka kwa mwingiliano wa watu na shughuli za kibiashara.
Soko Mkakati la Kahaza kata ya Rusumo wilayani Ngara
Kamati ya fedha ikikagua maeneo mbalimbali ya Jengo la Soko la kimkakati kahaza
Mhe Adroniz Bulindori Makamu Mkiti Halmashauri ya wilaya akiwa na mratibu wa LADP, Mhe Sudi Mkubila na wajumbe kamati ya fedha
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa