- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanafunzi wapatao mia nne (400) wa shule ya msingi Rusumo kata ya Murukulazo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, watakosa mahali pa kusomea baada ya madarasa manne kuezuliwa na upepo kwa wakati tofauti.
Taarifa hizo ni kwa mujibu wa mkuu wa Kaimu Mkurugezi Mtendaji na Afisaelimu Msingi Ndugu Gidion Samson Mwesiga alipoongea na Tovuti ya Halmashauri Oktoba 04, 2018; kwamba madarasa yaliyoezuliwa ni ya wanafunzi wa darasa la kwanza, la pili na la tatu.
“Siku chache zilizopita madarasa mawili yaliezuliwa na kupelekea wanafunzi wapatao mia mbili (200) kusomea chini ya miti; sasa madarasa mengine mawili yameezuliwa wanafunzi wengine watakosa mahali pa kusomea.” Alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji.
Kaimu Mkurugenzi huyo amesema upepo huo umetokea majira ya saa 8 mchana wakati wanafunzi wa darasa la nne walipokuwa wakifanya mitihani ya utimilifu ngazi ya mkoa, ambapo kila darasa lilikuwa na idadi yawanafunzi wapatao arobaini na wawili (42).
Alipoulizwa kama kulikuwa na madhara zaidi ya kuezuliwa kwa madarasa hayo; Kaimu Mkurugenzi alisema wanamshukuru Mungu kwani wanafunzi wote wako salama na hakuna madhara yoyote zaidi ya kuezuliwa kwa madarasa.
Amesema shule yake ni kama haipo kwani hata madarasa matatu yaliyobaki yaliwahi kuezuliwa, na kudai kwamba yanahitaji marekebisho makubwa; “kwa kifupi shule yangu haina miundo mbinu.” alisisitiza.
ili kuepuka madhara mengine ya aina hiyo, Kaimu Mkurugenzi ameagiza walimu wakuu na wakuu wa shule zote za msingi na za sekondari katika Halmashauri yaWilaya ya Ngara kupanda miti katika msimu huu wa mvua unaoanza hivi karibuni.
wakati Halmashauri inajipanga kufanya ukarabati wa madarasa hayo Kaimu Mkurugenzi amnewataka watendaji wa kijiji na kata wa kuitisha mkutano wa hadhara ili kujadili na kuona namna ya kurekebisha majengo hayo ili watoto wapate mahali pa kusomea kabla ya mvua kuanza.
Wakati huo huo, Mratibu wa Maafa Wilaya ambaye pia ni Afisa Mazingira wa Wilaya hiyo Ndugu Waziri Zawadi amewataka wananchi wilayani Ngara kupanda miti katika maeneo yao, ili kuepusha majanga ya upepo na kuongeza kwamba watu wanatabia ya kukata miti na kusahau kupanda mingine.
“Tukiendelea na tabia ya kuharibu mazingira hatutakuwa na njia rahisi ya kukwepa majanga kama haya, hata hivyo ni kumshukuru Mungu kwamba hakuna kijana aliyepoteza maisha katika tukio hili.” alisema mratibu huyo wa Maafa Wilaya.
Shule ya Msingi Rusumo ina wanafunzi zaidi ya mia saba (700), ambapo karibu nusu ya wanafunzi hao, hawana mahali pa kusomea kufutoa janga la upepo mkali ulioezua madarasa manne (04) kwa wakati tofauti.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa