- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika kipindi cha pili cha Awamu ya tatu ya mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF III) uliozinduliwa na Mhe. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania mnao Februari 2020 uliolenga kuziwezesha kaya kufanya kazi ili kujiongezea kipato kupitia utekelezaji wa miradi ya kutoa ajira za muda kwa walengwa.
katika kipindi hiki , TASAF imelenga kuwezesha kaya 6037 zinazopatikana katika vijiji 47 vya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ambapo shuguli mbalimbali zitafanyika kwa usimamizi wa wataalam watakaopatiwa mafunzo.
Katika mafunzo haya,lengo kuu ni kujenga uwezo kwa timu ya wataalam ngazi ya mamlaka ya eneo la utekelezaji kuhusiana na uibuaji,uandaaji,utekelezaji na usimamizi wa miradi ya kutoa ajira za muda. Mafunzo haya yaliyotolewa, yamejumuisha washiriki kutoka sekta mbalimbali zinazohusiana na miradi ya kutoa ajira za muda kwa walengwa ili kuhakiki uandaaji na utekelezaji miradi unazingatia viwango vya sekta na ubora unaokubalika.
Washiriki waliokusudiwa kushiriki ni 24 katika Halmashuri ya Ngara.
Mkufunzi aliyetoa mafunzo Bw. Ladislaus Mwamanga, aliwaasa washiriki wa mafunzo kuyapa umuhimu mafunzo waliyopatiwa ili waweze kutekeleza mpango huo kwa umakini na ukamilifu.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa