- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tar 20.10.2025 - Ngara
Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mhe Kanali Mathias Julius Kahabi, amewataka viongozi wa dini wilayani humo kusimama kidete kuhubiri amani wakati huu Taifa linapojiandaa kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Akizungumza katika kikao maalum kilichowakutanisha viongozi wa dini, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wadau wa amani, Col. Kahabi Dc Ngara amesisitiza umuhimu wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu kulinda amani ya nchi.
"Kila mmoja awe balozi wa mwenzake katika kuitunza na kuilinda amani ya nchi," alisema DC Kahabi.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa wananchi waliojiandikisha kujitokeza kwa wingi kupiga kura, huku akiwatahadharisha vijana dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
"Ninawakemea vikali baadhi ya vijana wanaotumia mitandao ya kijamii kusambaza matusi na ujumbe usio na maadili dhidi ya viongozi. Hili halikubaliki," aliongeza.
Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ngara, Kamanda William Solla, alisisitiza kuwa uhalifu wowote unaolenga kuvuruga amani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa uzito wake.
“Kosa la jinai halina ukomo. Watakaoshiriki vitendo vya uvunjifu wa amani watachukuliwa hatua kali za kisheria,” alionya Kamanda Solla.
Aliwataka viongozi wa dini kuhakikisha ujumbe waliopokea katika kikao hicho unawafikia waumini wao ili kwa pamoja kulinda misingi ya amani.
Naye Mgombea Ubunge Jimbo la Ngara,Dotto Jasson Bahemu ambaye alishiriki kikao hicho alisisiza kuwa uchaguzi ni haki ya kikatiba na si chanzo cha migogoro, hivyo Watanzania wote wanatakiwa kuungana pamoja kulinda amani, kuwa na upendo mshikamano na kuheshimu mamlaka zilizopo.
"Tuwakatae wote wenye nia ya kuchonganisha na kuvuruga amani ya nchi kwa kuhamasisha maandamano yenye madhara." alisema Dotto
Viongozi wote wa Dini waliohudhuria kikao hicho, wamekubaliana kwa pamoja kuilinda Amani ya Nchi na kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga Kura Oktoba 29,mwaka huu kuwachagua madiwani, Mbunge na Rais.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa